Katibu
Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo amesaini
kandarasi zenye thamani ya dola za Marekani Milioni 268.35 ambazo ni
zaidi ya Shilingi bilioni 600 za Tanzania mjini Tabora kwa mkopo wa
benki ya Exim ya nchini India kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzani
kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji kutoa Ziwa Victoria na kupeleka
katika Manispaa ya Tabora na Halmashauri za Igunga, Uyui, Shinyanga
Vijijini na Nzega.
Utekelezaji
wa mradi ni wa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ya Mradi ilikuwa
kufanya usanifu na kuandaa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi,
kazi ambayo ilifanywa na Kampuni ya WAPCOS Ltd ya India na ilikamilika
mwezi Desemba 2015.
Awamu
ya pili ni ujenzi wa mradi ambao umegawanyika katika sehemu tatu.
Sehemu ya kwanza itaanzia Kijiji cha Solwa (kilichopo Wilaya ya
Shinyanga Vijijini) hadi Mji wa Nzega, ujenzi utafanywa na Kampuni ya
Megha Engineering Infrastructures Ltd ya India. Sehemu ya Pili inaanzia
Mjini Nzega mjini hadi Manispaa ya Tabora kupitia Halmashauri ya Wilaya
ya Uyui, ujenzi utafanywa na Kampuni ya L&T ikishirikiana na kampuni
ya Shriram zote kutoka India.
Sehemu
ya tatu inaanzia Nzega mjini hadi Igunga mjini, ujenzi utafanywa na
Kampuni ya Afcons ikishirikiana na kampuni ya SMC zote kutoka India.
Usimamizi wa mradi unafanywa na Kampuni ya WAPCOS Ltd ya India.
Katika
hotuba yake Profesa Mkumbo alisema wakandarsi hao wameanza kazi leo
mara baada ya kusaini mikataba. “Wakandarasi wanaanza maandalizi yao leo
na kazi za ujenzi zitaanza mwezi Mei 2017 na muda wa kukamilisha mradi
utakuwa baada ya miezi 30”. Alisema Prof. Mkumbo.
Kwa
upande mwengine Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge,
alisema uchumi wa Viwanda hauwezekani bila uhakika wa maji, hivyo Wizara
yake itasimamia kwa kina juu ya uharaka wa mradi huo ili kuhakikisha
sera na dira ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda
inafanikiwa.
“Nitahakikisha
Wakandarsi hawa wanamaliza kazi kwa ubora na haraka kabla ya muda ili
kumuunga mkono Mheshimiwa Rais katika azma yake ya Tanzania ya viwanda,
kwasababu hakuna viwanda bila maji ya uhakika”, alisema Waziri Lwenge.
Na
serikali ya awmu ya tano ni serikali ya uwazi ndiyo maana nimeagiza
zoezi la kusaidi ujenzi wa miradi hii ifanyike hadharani ili ninyi
wananchi wenye miradi yenu muone, sasa mushirikiane na wakandari hao na
muwe walinzi wa vifaa ili kazi waifanye kwa haraka. Isitokee baadhi ya
wananchi wasio waaminifu kuhujumu vifaa vya ujenzi mambo ambayo
yatachelewesha mradi.” Alisisitiza Waziri Lwenge.
Pia
Lwenge aliwataka wakazi wa Tabora na maeneo mengine nchini watunze
vyanzo vya maji ili miradi hii ya maji iwe endelevu. Alisisitiza kuwa
sheria inakataza shughuli zote za kibinadamu kufanywa ndani ya mita
sitini kutoka kwenye chanzo cha maji.
“Tujiepushe
kufanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya mita 60, ili tuwe na
uhakika wa maji, tupande miti na kutunza mazingira yetu” alisema
mhandisi Lwenge.
Kwa
upande wao wabunge wa Tabora ambao mradi utapita katika maeneo ya
majimbo yao wameishukuru serikali kwa kutimiza ahadi yao ya muda mrefu
ya kuwaondolea kero ya uhaba wa maji katika maeneo yao.
Akieleza
umuhimu wa mradi huo, Mbunge wa Sikonge Joseph Kakunda alisema mradi
huu ni muhimu na mkombozi kwakuwa hamna vyanzo vya maji vya uhakika
katika maeneo mengi ya Mkoa wa Tabora.
Mbunge
Hussein Bashe aliomba wakandarasi wa ndani nao wafikiriwe ili waweze
kupata baadhi ya kazi ndogondogo (sub-contracts) ambazo zitasaidia
kukuza uchumi wa ndani na kuwajengea uwezo wakandarasi wetu nchini.
Akieleza
mafanikio ya mradi Profesa Mkumbo alisema kuwa, mradi ukikamilika
upatikanaji wa maji katika miji ya Tabora, Igunga, Nzega, Uyui pamoja na
baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini, unatarajiwa
kuongezeka kufikia asilimia 100 na wakazi zaidi ya milioni 1.1 watapata
huduma ya maji safi na salama.
Pia
alisema huduma bora ya maji itakayopatikana itachangia katika kuinua
uchumi kupitia maendeleo ya sekta nyingine zinazotegemea maji kama
Viwanda,Elimu, Utalii pamoja na kuimarisha huduma za afya wa wakazi wa
maeneo hayo.
Katibu Mkuu Wizara ya maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo na Visay Uplenchwar wa Kampuni ya Megha Engineering Infrastructures Ltd akisaini Mikataba ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka kijiji cha Solwa Shinyanga na kupeleka maji Nzega.
Picha ya pamoja Meza kuu pamoja na baadhi ya Wabunge wa Tabora.
Mbunge wa Nzega Hussein Bashe akimsalimia waziri wa Maji na Umwagiliaji Eng. Lwenge
Waziri wa maji na Umwagiliaji Eng. Gerson Lwenge akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakati alipowasiri katika viwanja vya Furahisha Tabora.
Mbunge wa Sikonge Joseph Kakunda akimpa mkono Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Post a Comment