Chelsea iliizaba Tottenham mabao 4-2 na hivyo basi kujikatia tiketi ya fainali ya kombe la FA dhidi ya mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Arsenal dhidi ya Manchester City.
Eden Hazard akishangilia bao
Willlian aliiweka mbele Chelsea kunako dakika ya sita kwa kupiga mkwaju wa adhabu kabla ya kuongeza la pili kwa njia ya penalti kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.
Harry Kane alikuwa amesawazisha kutoka kwa krosi iliopigwa na Christian Ericksen kwa Suprs ambao walisawazisha tena kupitia bao la Delle Ali.
Mchezaji wa ziada Eden Hazard aliiweka Chelsea mbele kwa mara ya tatu kabla ya Matic kufunga bao la nne na kuiweka kifua mbele Chelsea.
Post a Comment