NAIBU
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt, Juliana Palangyo,
(pichani anayezungumza), ametembelea miradi ya kuzalisha umeme wa Gesi Asilia ya upanuzi wa Kinyerezi I pamoja na ule wa Kinyerezi II.
Akizungumza
katika ziara yake ya kukagua miradi hiyo, Dkt Pallangyo ameridhishwa
sana na jitihada zinazofanywa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), katika kuhakikisha Miradi hiyo inakamilika kwa wakati, ambapo mpaka sasa ujenzi wa mradi wa kinyerezi II umefikia asilimia 53%.
“Niwapongeze
sana TANESCO kwa jitihada kubwa mnazozifanya katika kuhakikisha miradi
hii inakamilika kwa wakati, ambapo mmewezesha Majenereta 8 yenye jumla
ya Megawati (MW) 240 mpaka sasa yameshafika, hii ni hatua nyingine kubwa sana ,hivyo kupitia Mradi huu wa kinyerezi nina amini Tanzania ya Viwanda inawezekana”.
Akielezea
maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Kinyerezi II, Meneja wa Kituo hicho
Mhandisi Steven Manda alisema kuwa kituo hicho kinaendelea vizuri na
ujenzi katika kuhakikisha kinakamilika Desemba 2018, ambapo mpaka sasa
ukamilifui wa Mradi huo unategemea Kinyerezi I kutokana na Baadhi ya
mitambo kuingiliana hasa mitambo ya mfumo wa upozaji maji ambao utaunganishwa na mtambo wa Kinyerezi I.
Naye
Kaimu meneja wa Kituo cha Kinyerezi I Mhandisi Lucas Busunge amesema
kuwa Mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 150, Umeongezewa uwezo
wa kuzalisha Megawati zingine 185 ikiwa ni Awamu ya pili ya upanuzi wa
Mradi huo.
Kwa
ujumla miradi yote miwili itakapokamilika, jumla ya Megawati 575MW za
umeme utokanao na Gesi Asilia, zitazalishwa na kuunganishwa kwenye Gridi
ya Taifa na hivyo zitasaidia kuongeza upatikanaji wa Umeme wa Uhakika
na kuwezesha wananchi wengi kupata huduma
ya umeme na kufikia malengo ya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga
uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha Umeme unatumika kama njia moja wapo ya
kuleta maendeleo ya wananchi na kuinua vipato vyao binafsi na Taifa kwa ujumla. Naibu waziri Pallangyo alifanya ziara hiyo Aprili 20, 2017.
NAIBU
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt, Juliana Palangyo
akiongea na wanahabari alipotembelea miradi ya kuzalisha umeme wa Gesi Asilia ya upanuzi wa Kinyerezi I pamoja na ule wa Kinyerezi II.
Mafundi wakiendelea
na kazi katika moja ya jengo lilopo katika mradi wa kufua umeme wa gesi asili
megawati 240 wa Kinyerezi I ambapo unafanyiwa upanuzi.
Naibu katibu
Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo (wa pili kutoka
kushoto) akiambatana na viongozi wa TANESCO alipotembelea na kukagua maendeleo
ya ujenzi wa Miradi ya Umeme Kinyerezi I&II. Kushoto kwake ni kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
TANESCO Bi.Joyce Ngahyoma akifuatiwa na Kaimu Meneja Uhusiano Bw. Yasini Didas
Slayo Kulia pamoja na Meneja Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephen
Manda, (Kushoto)
Post a Comment