Juventus imefanikiwa kuingia katika hatua hiyo kwa kuitoa Barcelona ya Hispania kwa jumla ya mabao 3-0 ambayo walishinda katika mchezo wao wa kwanza wiki iliyopita huku katika mchezo wa jana wakitoka sare ya 0-0.
Nao Monaco wametinga hatua hiyo kwa kuitoa Borussia Dortmund kwa jumla ya mabao 6-3 ambapo katika mchezo wa kwanza walishinda magoli 3-2 na katika mchezo wa jana katika uwanja wao wa nyumbani wa Stade Louis II waliibuka tena na ushindi wa mabao 3-1.
Katika mchezo huo magoli ya Monaco yalifungwa na Mbappe dakika ya 3, Falcao dakika ya 17 na Germain dakika ya 81 huku goli la kufutia machozi la Dortmund likifungwa na Reus dakika ya 48.
Post a Comment