Chameleone kuachana na Mke wake wa Miaka 10
Daniella Atim, ambaye ni mke wa Hitmaker na muimbaji kutoka Uganda, Joseph Mayanja, maarufu kama Chameleone, amewasilisha ombi la kutaka hakimu katika moja ya mahakama nchini Uganda kuivunja ndoa yake na hitmaker huyo.
Daniella ameeleza sababu za kutaka kuachana na Chameleone zikiwa ni pamoja na kupigwa na muimbaji huyo pamoja na kunyanyaswa yeye na watoto wake.
Daniella na Chamelone wameoana kwa zaidi ya miaka kumi na kufanikiwa kupata watoto wanne pamoja.
Hatua za kumpata Chameleone kutolea ufafanuzi suala hili, hazijafua dafu.
Post a Comment