Home
»
habarizakitaifa
» BARABARA YA VIGWAZA-BUYUNI-MWAVI YAHARIBIKA VIBAYA/RIDHIWANI AAHIDI KUSIMAMIA KERO HIYO
MBUNGE
wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,akiangalia barabara kutoka
Vigwaza-Mwavi iliyoharibika vibaya eneo la Buyuni hali inayosababisha
magari kushindwa kupita.
Mkazi wa Mwavi ,Zainab Zuberi akivushwa kwenye maji yaliyokata barabara eneo la Buyuni,kwa kubembwa shingoni .
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,akizungumzia kero ya kuharibika
kwa baadhi ya miundombinu ya barabara kutokana na mvua zinazoendelea
kunyesha,ambapo mvua iliyonyesha april 7 na 8 imesababisha kuharibu
barabara ya Vigwaza-Buyuni-Mwavi na ya Milo-Kitonga-Ruvu.
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
MVUA
kubwa iliyoambata na upepo mkali,imekata mawasiliano ya miundombinu ya
barabara eneo la Buyuni, na kusababisha wakazi kutoka kata ya Vigwaza na
Mwavi jimbo la Chalinze,kupata shida.
Hali
hiyo inasababisha wakazi hao,kuvushwa kwa kupata msaada wa kubebwa
mgongoni na shingoni kwa gharama ya sh.3,000 na 2,000 na pikipiki
kupitishwa kwa sh.5,000 huku magari yakishindwa kupita kabisa.
Baadhi ya wakazi hao,akiwemo Zaina Zuberi aliekuwa akienda Mwavi,alisema wapo katika hali ngumu .
“Mvua
hapa bado haijanyesha,maji haya yanatokea maeneo ya Msoga huko na
kufika huku daraja la Mbiki,Buyuni na kukatiza katika hii
barabara,sipati picha mvua ikipiga hapa kwa mwezi huu”
“Barabara
ni mbovu kama mnavyojionea,haipitiki,watu tunapata shida kufuata
mahitaji ya nyumbani ,tatizo ni mkandarasi ,barabara imejengwa bila
kuwekwa makaravati,kila akielekezwa kujenga kutokana na hali halisi ya
barabara haiwi hivyo,”
Nao
baadhi ya vijana wanaosaidia kuwavusha watu na pikipiki,akiwemo Rashid
Juma,alisema tangu mvua ziharibu eneo hilo april 7 wanavusha watu kwa
maelewano kulingana na uwezo wa mtu.
“Tunapata fedha kulingana na kichwa cha mtu au pikipiki,kila mtu mmoja 3,000 au 2,000 na pikipiki 5,000 “alieleza.
Aidha kutokana na mvua hizo,zimeathiri pia barabara nyingine ya kutoka Milo-Kitonga hadi Vigwaza.
Mbunge wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete ,alitembelea barabara hizo na kujionea hali halisi.
Ridhiwani
alisema ,hali iliyopo hairidhishi na kuwapa wakati mgumu wakazi wa
maeneo hayo,na ameahidi kuisimamia kero hiyo kwa kuifikisha bungeni na
halmashauri ya wilaya ya Chalinze ili lifanyiwe kazi.
Alieleza
kuna kila sababu ya mkandarasi kufanya kazi kulingana na uhalisia wa
eneo husika hali inayosababisha wananchi kupata tabu na barabara
kuharibika kila wakati.
Katika
hatua nyingine Ridhiwani ,aliunga mkono juhudi za ujenzi wa darasa
lililobomoka kutokana na mvua iliyonyesha april 7 ambapo amechangia
kiasi cha sh.100,000,mabati 50,mifuko ya saruji 50 na nondo 20.
Alibainisha kwamba shule hiyo imejengwa miaka 40 iliyopita hivyo miundombinu yake pia imechakaa.
Ridhiwani alisema kuna kila sababu ya kuangalia namna ya kukarabati shule hiyo kwani majengo yake yamejengwa miaka mingi.
Afisa
mtendaji wa Kidogozero,Lilian Mbwa,alisema kila kaya itachangia
matofali mawili na kila mjumbe wa serikali ya kijiji ni tofali 10.
Hata hivyo alisema halmashauri ya kijiji itachangia jumla matofali 200 na wadau wa maendeleo matofali 300.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita,kaya zaidi ya 20 zimekosa makazi ya kuishi na nyumba
zaidi ya 90 ziliharibika ,kubomoka na nyingine kuezuliwa mapaa huko
jimbo la Chalinze,kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali.
Maeneo
yaliyokumbwa na adha hiyo ni Chalinze Mzee,Bwawa la umwangiliaji la
Msoga ambalo limetoboka ,Msoga na shule ya Sekondari ya Imperial.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Related Posts
- Zanzibar to Organize a Half Marathon race to Promote Gender Mainstreaming, Attain Sustainable Development Goal06 Jan 20180
More than 300 Zanzibari women, men, girls and boys are expected to participate in t...Read more »
- Embassy of Kuwait in Tanzania Committed to Support Educational Projects in Zanzibar18 Dec 20170
Member of the House of Representative in Zanzibar, Hon Simai Mohammed Said in discussion ...Read more »
- Turkey to intensify relationship with SUZA16 Aug 20170
Delegation of Presidency for Turks Abroad and Related Communities (YTB) meets Prof. Rai (...Read more »
- RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH WATEMBELEA KUWAJULIA HALI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM28 May 20170
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamo...Read more »
- Halmashauri kunufaika na Tsh 250 bilioni za mradi wa maji vijijini18 May 20170
Halmashauri za wilaya zimetakiwa kuongeza ufanisi katika kusimamia miradi ya maji kwa kucha...Read more »
- NAIBU MKURUGENZI WA IMF AKUNWA NA UKUAJI WA UCHUMI WA TANZANIA, AAHIDI KUFUNGUA DIRISHA LA MIKOPO KWA TANZANIA18 May 20170
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kulia) akiel...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.