WAZIRI MKUU ANUSA MADUDU MINADA YA MADINI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisisitiza jambo katika kikao alichokiitisha kuhusu masuala ya madini kati
yake na viongozi wa Serikali, viongozi wa kampuni ya uchimbaji madini
ya Tanzanite One na baadhi ya wachimbaji wadogo ,kwenye Makazi yake
Oysterbay jijini Dar es salaam jana Februari 27, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao alichokiitisha kuhusu
masuala ya madini kati yake na viongozi wa Serikali, viongozi wa kampuni
ya uchimbaji madini ya Tanzanite One na baadhi ya wachimbaji
wadogo,kwenye makazi yake, Oysterbay jijini Dar es salaam jana Februari
27, 2017.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo alipokuwa akifafanua jambo katika kikao kilichoitishwa
na Waziri Mkuu kwenye Makazi yake Oysterbay jijini Dar es salaam
Februari 27, 2017, kwa ajili ya kujadili masuala ya madini. Watatu
kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na ni Mkuu wa
Mkoa wa Manyara Dkt. Joel Bendera.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
*Amuagiza Kamishna wa Madini aende Mererani
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema anafuatilia kwa makini minada ya madini
inayofanyika nchini kwa sababu anazo taarifa za kukiukwa utaratibu
kwenye minada hiyo.
Amesema
ukiukwaji huo unachangia kutobadilika kwa mapato ya mauzo yatokanayo na
mnada hata kama kuna vito viliyokakatwa au havijakatwa.
Ametoa
kauli hiyo jana jioni (Jumatatu, Februari 27, 2017) wakati akihitimisha
kikao alichokiitisha kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam
kilichojumuisha Mawaziri wa Fedha pamoja na Nishati, Mkuu wa Mkoa wa
Manyara na watendaji wake, Mbunge wa Simanjiro, wamiliki wa mgodi wa
Tanzanite One, watumishi waliofukuzwa kazi na wachimbaji wadogo.
Alisema
licha ya kuwa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha
Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT) kinasifiwa kwa kuongeza mapato ya
madini, bado kuna kazi ya ziada inabidi ifanyike kwenye minada hiyo ili
Serikali iweze kunufainika na madini hayo.
“Uzoefu
wa kwenye minada ya korosho unaonyesha kuwa wanaushirika ndiyo wanaiba
fedha za wakulima. Nimekuwa ninafuatilia kwa muda sasa uendeshaji wa hii
minada na sijaridhishwa na uendeshaji wake. Hakuna tofauti ya bei
madini ya Tanzanite yanapokuwa yamekatwa au la,” alisema.
Kwa
mujibu wa wataalamu wa madini na vito, inapotokea kuna madini yamekatwa
bei inapaswa kuwa juu ikilinganishwa na madini ghafi yanapouzwa moja
kwa moja.
Amemuagiza
Kaimu Kamishna wa Madini, Bw. Benjamini Mchwampaka (ambaye alihudhuria
kikao hicho kwa niaba ya Kamishna wa Madini) aende Mererani na
kufuatilia utendaji kazi wa mgodi wa Tanzanite One na suala zima la
teknolojia zinazotumika kiwandani hapo.
Waziri
mkuu aliitisha kikao hicho kufuatia ahadi aliyoitoa kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika Mererani, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara
Februari 16, 2017 kwamba akimaliza ziara ya mkoa huo ataitisha kikao na
wawekezaji wa Tanzanite One baada ya kupokea malalamiko kwamba hali ya
watumishi ilikuwa nafuu wakati kampuni hiyo ilipokuwa inamilikiwa na
wazungu kuliko ilivyo hivi sasa.
Ili
kuhakikisha ukusanyaji wa mapato katika sekta ya madini unaongezeka,
Waziri Mkuu amemwagiza Kamishna wa Mamlaka ya Mapato (TRA) aimarishe
ukaguzi kwenye viwanja wa ndege vya Arusha na Kilimanjaro (KIA),
“Kamishna
wa TRA na watu wako inabidi mjipange kwa sababu kuna njia nyingi za
ukwepaji kodi zinafanyika kwenye sekta ya madini wakiwemo hata hawa
wachimbaji wadogo. Simamieni utaratibu wa kufuatilia kodi, nendeni kule
walipo, msisubiri waje kuwaletea malipo ofisini. Wasipokuja je? Au
wakija wakakuta mmetoka ofisini je?” Alihoji Waziri Mkuu.
Akizungumzia
kuhusu uelewa wa sheria miongoni mwa wachimbaji wadogo, Waziri Mkuu
alisema Wizara ya Nishati na Madini kupitia kwa Kamishna wa Madini
wanapaswa kutoa elimu na uelewa wa kisheria kwa wachimbaji hao ili
kupunguza migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza kwenye maeneo mengi
nchini.
“STAMICO
na Kamishna wa Madini fanyeni kazi pamoja, waelewesheni wachimbaji
wadogo kuwa uwepo wa vitalu maana yake kuna mipaka ambayo pia inajumisha
utoaji wa leseni kwa wenye vitalu hivyo. Kwa hiyo, waelimisheni kuwa
mtu hapaswi kwenda upande wa pili wa mtu mwenye leseni, akifanya hivyo
atakuwa anavunja sheria.”
“Ninyi
ni wadau wakubwa wa sekta hii kwa hiyo mnapaswa kushiriki katika zoezi
la kutoa elimu. Mnayo maeneo mengi ya uchimbaji lakini yana migogoro,
mfano ni kule Ngaka na Kiwira. Maeneo yote haya yanahitaji usimamizi
mzuri. Mnayo Bodi, Mwenyekiti yupo kwa hiyo mnatosha kuifanya kazi hii,”
alisisitiza.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa mgodi wa Tanzanite
One waboreshe mahusiano yao na vijiji vilivyo jirani na mgodi huo.
“Kuweni karibu na wananchi ili wajue umuhimu wenu na uwepo wenu na
waweze kusaidia kulinda mali zenu. Shirikianeni na Halmashauri na Baraza
la Madiwani, tangazeni kazi zenu za CSR ili wananchi wajue mmechangia
nini katika kusaidia maendeleo yao,” alisema.
Kuhusu
suala la watumishi waliofukuzwa kazi kwenye mgodi huo, Waziri Mkuu
amemwagiza Katibu Mkuu (OWM-Kazi, Ajira na Vijana), Bw. Erick Shitindi
asimamie suala lao na kuwapatia majibu kuhusu hatma ya suala hilo.
Watumishi
hao walikuwa wanawakilisha wenzao 201 ambao walifukuzwa kazi Februari
8, 2016 kwa sababu ya kufuatilia maslahi yao vikiwemo malipo ya saa za
kazi za ziada (overtime), mishahara ya miezi miwili, malipo ya NSSF,
vitendea kazi na usalama wa kazi migodini.
Post a Comment