Eric Cantona anyoosha mikono juu kwa Zlatan Ibrahimovic
Baada ya mchezaji wa zamani wa Manchester United, Eric Cantona kuonekana kutoufurahia usajili wa Zlatan Ibrahimovic mwanzoni mwa msimu huu huku akimrushia maneno ya kashfa mchezaji huyo – hatimaye amemnyooshea mikono juu.
Cantona amesema Ibrahimovic amethibitisha kuwa yeye ni mchezaji mkubwa hiyo ni baada ya mshambuliaji huyo kuisaidia Man United kushinda kombe la EFL Jumapili hii.
“He’s a great player with a strong personality. He played for Milan and Barcelona so he knows and understands the pressure. He has proved he is also a great man because there are two type of old player, the one which does not like the young players, and can destroy them,” Cantona ameuambia mtandao wa Manchester Evening News.
Cantona aliwahi kumkejeli mchezaji huyo kwa kumwambia hawezi kuwa mfalme ndani ya timu hiyo labda achague kuwa mtoto wa mfalme. “Just one last thing, there can only be one King in Manchester. You can be the Prince if you want to. And the No 7 is yours if you are interested. That is my welcome gift to you… The King is gone! Long live the Prince!,” hii ni kauli aliyowahi kuitoa Cantona kwa Zlatan.
Lakini siku chache baadae kupitia gazeti la gazeti la Aftonbladet, Zlatan alimjibu wa kusema, “I won’t be King of Manchester. I will be God of Manchester.”
Post a Comment