Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Wabogojo aingia kwenye maisha mapya ya ndoa
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Orodha ya mastaa wanaoukimbia ukapera inazidi kuongezeka. Mchekeshaji na mcheza sarakasi maarufu nchini Wabogojo naye amefunga...


Orodha ya mastaa wanaoukimbia ukapera inazidi kuongezeka. Mchekeshaji na mcheza sarakasi maarufu nchini Wabogojo naye amefunga ndoa Ijumaa hii na mpenzi wake wa muda mrefu.

Kupitia mtandao wa Instagram, mchekeshaji huyo ameweka picha akiwa na mke huyo wakati wa ndoa hiyo na kuandiaka:
Mwisho: Rasmi Mume & Mke. Asante Mungu, nimebarikiwa kwa jambo hili, #Alhamdullilah! Familia yangu kwa ujumla & upande wa mama, sina cha kuwalipa kwa upendo na ushirikiano wenu; Nawapenda! Wafanyakazi wenzangu, ndugu zangu, rafiki zangu na kila mmoja, kutoka ndani ya moyo wangu; Nawashukuru sana. Kwa mke wangu mpendwa……..Nashukuru kwa kunikubali kwa hivi nilivyo, Nakuita mke wangu sasa! Asante mke wangu na upendo wangu kwako hauna mwisho!

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top