Vanessa Mdee aachiwa kwa dhamana
Baada ya kushikiliwa na polisi kwa takriban siku 4, Vanessa Mdee ameachiwa kwa dhamana Jumatatu hii.
Vanessa ambaye alishikiliwa muda mfupi baada ya kurejea kutoka Afrika Kusini ni miongoni mwa mastaa waliotajwa kwenye orodha ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana kuhusishwa na matumizi na biashara ya dawa za kulevya.
Inadaiwa kuwa Vee anatetewa na mwanasheria maarufu, Peter Kibatala.
Watu wengi wakiwemo mastaa nchini walikuwa wakimtetea kutaka kuachiwa huru kutokana na kile wanachoamini kuwa anaonewa.
Post a Comment