Mwanasheria wa rais wa Marekani, Donald Trump amemjia juu msanii wa muziki wa hip hop, Snoop Dogg baada ya kuachia video yake mpya ya ‘Lavender’ akiwa anamwonyeshea bastola Donald Trump wa uwongo ambae ametumika ndani ya video hiyo.
Michael Cohen ambaye ni mwanasheria wa Donald Trump kupitia mazungumzoyake aliyoyafanya na mtandao wa TMZ, alifunguka kwa kusema kwamba kitendo ambacho amekifanya Snoop Dogg ni udhalilishaji kwa Rais Donald Trump na kusema kwamba Snoop anapaswa kuomba msamaha kwa kitendo chake hicho.
Ni sawa kufanya utani lakini kwa upande wa Snoop Dogg amevuka mipaka ya utani kwa kile kikubwa ambacho alikifanya cha kutoa pisto ya uongo na kuinyoosha kwa mfano huo wa Donald Trump huku ikiwa imeandikwa ‘Banng’, Cohen anasema kwamba hakuna utani wa mauaji kwa Rais na kitendo hiko kimemshtua sana mwanasheria huyo wa Trump.
“Nisingeweza kulikubali jambo hilo hata kama Raisi angekuwa ni Barack Obama, na vilevile siwezi kukubali hata kwa Donald Trump, unajua kitu ambacho kinanisikitisha kwa Snoop Dogg ni kwamba kuna vitu vingi sana ambavyo angeweza kuvifanya kwa jamii lakini sio kwa video hii” aliongea Michael Cohen.
Hii ndio video ambayo Mwanasheria wa Trump hajaipenda
Post a Comment