Leicester City yajitengenezea rekodi ya Uefa, yatinga robo fainali kwa kishindo
Timu ya soka ya Leicester City ya Uingereza imejitengenezea rekodi yake baada ya kufanikiwa kuingia katika hatua ya robo fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya (Uefa).
Leicester imetinga hatua hiyo baada ya kuifunga Sevilla ya Hispania mabao 2-0 usiku wa Jumanne hii na kufanya matokeo ya jumla kuwa 3-2.
Magoli ya timu hiyo yalifungwa na Wes Morgan dakika ya 27 na Marc Albrighton dakika ya 54. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa wiki mbili zilizopita Sevilla walishinda mabao 2-1 katika uwanja wao wa Ramón Sánchez Pizjuán.
Katika mechi nyingine iliyochezwa usiku huo Juventus walifanikiwa kuingia katika hatua hiyo baada ya kuifunga FC Porto 1-0 na kufanya matokeo ya jumla kuwa 3-0. Mechi nyingine zitachezwa leo (Jumatano) ambapo Atletico Madrid itacheza na Bayer Leverkusen na Monaco dhidi ya Manchester City.
Post a Comment