Profesa Jay aahidi kuachia kitu kipya Jumatano hii
Rapper mkongwe wa hip hop nchini Profesa Jay ameahidi kuachia wimbo wake mpya Jumatano hii.
Ni miezi saba imepita tangu rapper huyo alipoachia wimbo wake wa ‘Kazi Kazi’ ambao bado unazidi kufanya vizuri sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye redio na runinga. Kupitia mtandao wa Instagram, Jay ameahidi kuachia wimbo huo ikiwa ni audio pamoja na video.
“The Wait is Over….Jumatano Tar 15 March Naangusha MZIGO MPYA kwa watu wangu wa nguvu.#KIBABE (The ICON) Stay tuned on your favourite Radio and TV stations ,” ameandika Profesa kwenye mtandao huo.
Post a Comment