Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Mkwasa afunguka ishu ya beki wa Yanga Vicent Bossou kudai mishahara ya miezi minne
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya kuzagaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii zikidai beki wa Yanga, Vicent Bossou hajalipwa mishahara ya miezi minne, K...


Baada ya kuzagaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii zikidai beki wa Yanga, Vicent Bossou hajalipwa mishahara ya miezi minne, Katibu mkuu wa Yanga amefunguka na kuzungumzia sakata hilo.

Siku chache baada ya mechi ya Yanga na Simba, ulisambaa ujumbe unaodaiwa kuwa wa beki huyo ukionyesha kulalamika kwamba hajalipwa mishahara ya miezi minne.
Jumatano hii Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amefunguka kwa kudai kuwa sio kweli kwamba mchezaji huyo anadai mshahara wa miezi minne.
“Bossou haidai Yanga SC mishahara ya miezi minne kama habari zinavyotembea . Check za mishahara ya beki huyu kwa siku 10 mwezi wa 12 na January zilikwisha andaliwa na mtoa check amemueleza kuja kuchukua lakini sielewi kwa nini hakuzifuata,” ilisema taarifa hiyo kutoka kwenye mtandao wa klabu hiyo.
“Kabla ya mechi na Simba SC alifanya vizuri mazoezi lakini kwa taarifa zilizopo aliondoka mazoezini bila ruksa ya mwalimu . Tunasubiri ripoti ya mwalimu kwa ajili ya kuchukua hatua,” aliongeza Mkwasa.
Katibu mkuu huyo hivi karibuni alitoa taarifa ya kuwa klabu hiyo kwa sasa inatatizo la kiuchumi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top