MEYA ILALA AFUNGUA RASMI DARAJA LA BONYOKWA-KINYEREZI
Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonesti (Chadema) akihutubia wakati wa ufunguzi wa daraja hilo
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akikiwa
amekata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi daraja linalounganisha
Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini
Dar es salaam.
Mwandishi wetu
MSTAHIKI
MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko jana alifungua
rasmi daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi
katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam.
Awali
akizungumza katika hafla hiyo Mhandisi wa Manispaa ya Ilala ndugu
Benjamin Maziku alisema daraja hili limejengwa kwa takribani mwaka
mmoja na kugharimu Tsh.million 478 hadi kukamilika kwake leo hii.
Ujenzi wa daraja hili umesua sua kwa siku nyingi kutokana na sababu
mbali mbali lakini kutokana na usimamizi imara wa Mstahiki Meya wa Ilala
Mhe. Charles Kuyeko sasa historia imebadilika.
Meya
Kuyeko akizungumza na umati wa wananchi waliokusanyika kushuhudia
ufunguzi huo amewasitiza kulilinda na kulitunza vyema daraja hilo kwani
limejengwa kwa kodi zao.
Awali,
Meya akitoa historia ya daraja hilo amesema kuwa, waliokuwa wanatakiwa
kujenga daraja hilo ni wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) lakini
kutokana na kusuasua kwao, Mimi (Meya) niamua kuingilia kati kwa
Manispaa kutenga Fedha kujenga daraja la muda ili kuwasaidia wananchi wa
Bonyokwa kuondokana na atha ya kuwa Kisiwa hususani wakati wa Mvua.
Kuyeko
ambaye pia ni Diwani wa kata ya bonyokwa amewaambia wananchi hao
waliofurika kwenye uzifunguzi huo kuwa huo ni mwanzo tu wa utekelezaji
wa ahadi zake katika kutatua kero za wananchi na wapiga kura wake.
"Nawahakikishia kuwa hamtajutia kunipa kura zenu kwani daraja hili
imekuwa kero ya miaka nenda rudi lakini Mimi nimeimaliza kwa muda mfupi
kwa kushirikiana na watendaji wangu hivyo mtarajie mengi kabla mwaka huu
kuisha hata daladala zitakuwa zinafika hadi kisiwani".
Mbali
na hayo,Meya amewaahidi wananchi hao muda mfupi ujao atatatua kero ya
maji na barabara kama ambavyo aliahidi kutekeleza wakati wa kampeni.
Ufunguzi
huo ulihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa kiserikali na kisiasa
akiwemo mbunge wa Viti Maalum Mhe. Anatropia Theonest, madiwani wa kata
mbalimbali na viongozi wa vyama vya siasa.
Akitoa
salam kwa niaba ya viongozi wa vyama vya siasa, Dk.Makongoro Milton
Mahanga mbunge wa zamani jimbo la Segerea ambaye kwa sasa ni, Mwenyekiti
wa CHADEMA Mkoa wa Ilala alisema, "Tangu niwe kiongozi sijawahi kuona
kiongozi mahiri kama Meya Kuyeko.
Ameweza
kuwaunganisha viongozi wa Manispaa yake na kuwa kitu kimoja, na hadi
sasa ameshafanya vitu vingi ambavyo awali vilishindikana nakupongeza
sana Meya Kuyeko.
Dkt.
Mahanga aliwasisitiza wananchi kuwaamini viongozi wanaotokana na UKAWA
kwani ni wazuri jifunzeni kwa Kuyeko mambo makubwa anayoyafanya. Kwa
niaba ya Chadema nampongeza sana Meya Kuyeko kwa kukiwakirisha vyema
chama kwa wananchi.
Naye
Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Segerea ndugu Gango Kidera aliwataka
wananchi wa Bonyokwa waendelee kumwamini na kumuunga mkono Meya Kuyeko,
Baraza lake la Madiwani kwani amekuwa mfano bora kwa kutekeleza ahadi
zake zinazotokana na ilani na Sera za Chadema/UKAWA.
Chadema
imemtuma Kuyeko kuwatumikia wananchi wa Bonyokwa na Manispaa nzima ya
Ilala kwa kuhakikisha anatatua kero zao kwa spidi ya mwendokasi na leo
tumeona anatenda kwa maslahi ya wananchi. Nakupongeza sana Meya Kuyeko,
alisema Kidera
Viongozi
wengine waliozungumza katika ufunguzi huo ni Mbunge wa Viti Maalum Mhe.
Anatropia Theonest ambaye aliwapongeza wananchi wa Bonyokwa kwa
kumchagua Kuyeko, wananchi wa Bonyokwa mlifanya maamuzi sahihi kuchagua
Chadema kwa sababu bila Chadema Meya Kuyeko tusingempata.
Anatropia
pia alimpongeza Meya Kuyeko kwa kuendelea kutatua kero za wapiga kura
wa Bonyokwa siku hadi siku na Ilala kwa ujumla. UKAWA kwa Manispaa ya
Ilala chini ya Meya Kuyeko imeleta matumaini makubwa kwani wakazi wa
Manispaa wapatao 1,415,443 walikuwa wamekata tamaa kabisa kwani viongozi
waliopita walishindwa kutatua kero za wananchi, hivyo UKAWA chini ya
Meya Kuyeko ni mfariji mkuu wa wananchi, alisema Anatropia.
Diwani
wa Buguruni Mhe. Penza wa CUF akizungumza kwa niaba ya Madiwani wa
Ilala alisema ilani ya UKAWA imeweka vipaumbele kwenye Barabara, maji,
afya, elimu, na masoko na mitaji hivi vyote vinafanyika.
Meya
Kuyeko aliwashukuru wananchi kwa kuendelea kumwamini na kumpa
ushirikiano wa karibu hali ambayo inampa ari ya kuwatumikia kwa nguvu
zake zote. Pia amekishukuru chama chake Chadema, viongozi, Madiwani na
watendaji wote wa Manispaa ya Ilala wakiongozwa na Mkurugenzi kwa kumpa
ushirikiano wa hali na Mali katika kuwatumikia wananchi.
Post a Comment