Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Lady Gaga achukua nafasi ya Beyonce kutumbuiza kwenye Coachella
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya wiki iliyopita Beyonce kulazimika kusitisha kwenda kutumbuiza kwenye tamasha la Coachella Valley Music and Arts, mwaka...


Baada ya wiki iliyopita Beyonce kulazimika kusitisha kwenda kutumbuiza kwenye tamasha la Coachella Valley Music and Arts, mwaka huu kutokana na kuwa mjamzito Lady Gaga amedondokewa na shavu hilo.

Kupitia mtandao wa Twitter, Gaga amethibitisha kutumbuiza kwenye tamasha hilo kwa kuweka cover la tangazo lake na kuandika, “Let’s party in the desert! .”

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Jumamosi ya April 15 katika viwanja vya Empire Polo, Indio mjini California ambapo wasanii kama Kendrick Lamar, Radiohead, The XX, Justice, Lorde, Father John Misty, Bon Iver na wengine wanatarajiwa kutumbuiza.
Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa Queen Bey akashiriki kwenye tamasha kama hilo la mwakani. Inadaiwa kuwa tamasha la Coachella ndio linaongoza kuingiza fedha nyingi duniani.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top