KAMATI YA UTALII WATEMBELEA YALIYOKUWA MAFICHO YA MWALIMU NYERERE WAKATI WA HARAKATI ZA UHURU MKOANI MBEYA
Kamati
ya Utalii ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya ikiongozwa na Afisa Utalii wa
Jiji Bi.Levina Modest na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Geofrey Kajigili
wanaofanya kampeni hii kabambe ya utambuzi wa Vivutio vyote vilivyopo
Jijini Mbeya kwa kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali za Uyole
Cultural Tourism Enterprise pamoja na Elimisha .
Pia
wamemtembelea Mzee Mkongwe wa Siasa nchini, Mzee Rashid Ally Sinkala
ambaye amewahi kuwa Diwani wa iliyokuwa ikiitwa Kata ya Soko Matola
(sasa Kata ya Maendeleo) kwa miongo kadhaa,na amewahi kutumika kama Meya
ya Halmashauri ya Mbeya Mjini.
Mzee
Sinkala ameiambia Kamati ya Utalii kuwa Miaka zaidi ya 50 iliyopita
wakati wa Siasa za Ukombozi wa Tanganyika enzi za Chama cha Tanganyika
African National Union (TANU)Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
alikuwa akifikia kwenye nyumba ya mwanasiasa Mkongwe mwanamke
aliyejulikana kwa majina ya Zaituni Binti Matola.Binti Matola alitenga
chumba kimoja nyumbani kwake kama Maficho ya Mwalimu Nyerere.
Mzee
Sinkala akiwa mlangoni mwa Chumba maalum alipokuwa akifikia Mwalimu
Nyerere ndani ya nyumba ya muasisi wa TANU na mwanamke mashuhuri Hayati
Zaituni Binti Matola aliyesababisha maeneo hayo kuitwa "Soko Matola"
Jijini Mbeya
Wajumbe
wa Kamati ya Utalii Jijini Mbeya wakimsikiliza kwa makini Meya mstaafu
wa Halmashauri ya Mbeya Mjini Mzee Sinkala ndani ya nyumba ya kihistoria
ya Binti Matola.
Post a Comment