Haya ndio Majina 26 ya kikosi cha Taifa Stars
Kocha wa timu ya Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza kikosi chake kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki.
Stars inaweza kucheza na kati ya Zambia na Rwanda au timu nyingine kwa kuwa kumekuwa na taarifa tofauti.
Kikosi hicho cha Mayanga ambacho kimeongozwa na nahodha Mbwana Samatta anayekipiga nchini Ubelgiji katika klabu ya KRC Genk kimekuwa na vijana wengi zaidi.
Makipa;
Aishi Manula (Azam), Deogratius Munishi ‘Dida’ (Yanga) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
Mabeki;
Shomari Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Yanga), Mohammed Zimbwe ‘Tshabalala’ (Simba), Gardiel Michael (Azam), Andrew Vincent (Yanga), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba) na Erasto Nyoni (Azam FC).
Viungo;
ni Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam), Said Ndemla (Simba), Frank Domayo (Azam), Muzamiru Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga), Shiza Kichuya (Simba), Farid Mussa (DC Tennerife) na Hassan Kabunda (Mwadui FC).
Washambuliaji;
Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna, Sweden), Ibrahim Ajibu (Simba), Mbarak Yussuf (Kagera Sugar) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting).
Post a Comment