Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Idri Sultan akubali Jokate ni mwanamke wa shoka
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Jokate Mwegelo ni mwanamke wa shoka. Idris Sultan amempongeza mrembo huyo kwa kufanya makubwa kwa jamii kwa kubadilisha maisha...


Jokate Mwegelo ni mwanamke wa shoka. Idris Sultan amempongeza mrembo huyo kwa kufanya makubwa kwa jamii kwa kubadilisha maisha ya vijana takribani laki tano ndani ya kipindi kifupi japo wengi wanajifanya kufumba macho na kuziba masikio kwenye hilo.

Kupitia mtandao wa Instagram, Idris ameandika:
Ndani ya miaka 5 she has done so much more than any celebrity in Tanzania kwenye jamii. Naomba nihamishie upepo kwake kwa shukrani zote kwa yote aliyoyafanya kuinyanyua jamii ya watanzania na naomba msamaha kwa niaba ya watanzania kwani tulikua busy tunaangalia nani anatoka na nani na nani kagombana na nani na nani kaposti uchi leo, tukasahau kua umebadilisha maisha ya vijana zaidi ya laki 5 ndani ya miaka miwili tu. Ingekua muamuzi ni mimi ungekua Forbes because ni celebrity pekee uliyesimamisha brand product yako kwa jina lako and yes African boy ya Jux inakuja pia. Uliyoyafanya kwenye jamii yako bila kulazimishwa ni zaidi ya baadhi viongozi tuliowachagua kufanya kazi hizo tunazowalipa kufanya. If am allowed may I please say you are “THE FLOWER OF TANZANIA” if you ask me why its because you are beautiful and you make us smell good werevaa you go.
Kwa niaba ya watanzania ningependa kusema tumejisahau sana na tusamehewe. Stay beautiful .. cc: @jokatemwegelo #TheFlowerOfTanzania

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top