Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Hii ndio sababu ya Temba kukaa kimya kwa muda mrefu kwenye muziki
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Mh Temba amefunguka sababu ya kukaa kimya kwa muda mrefu kwenye muziki. Msanii huyo amekiambia kipindi cha FNL cha EATV kuw...


Mh Temba amefunguka sababu ya kukaa kimya kwa muda mrefu kwenye muziki.

Msanii huyo amekiambia kipindi cha FNL cha EATV kuwa alitakiwa kuachia wimbo mpya mapema kabala hata ya ‘Acha Waoane’ wa Chege lakini kuna vitu viliingiliana vikavuruga ratiba hiyo.
Temba amevitaja vitu hivyo ni pamoja na kuibiwa fedha zake na zingine za baadhi ya marafiki zake ambazo alitegemea kufanyia kazi kwenye muziki ikiwemo kutumika kwenye kutengenezea video.
Rapper huyo amemtaja aliyewaibia anaitwa Mustafa Andumbotela Ndingubita na ameahidi kutoa kiasi cha milioni moja kwa mtu atakayesaidia kukamatwa kwake huku naye Chege akiongezea kiasi cha laki tano kwenye zawadi hiyo ambapo itakuwa ni milioni moja na nusu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top