Clouds 360 wamkabidhi Jetman milioni 15
Watangazaji wa kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV wakiongozwa na Babbie Kabae na Sam Sasali wamemkabidhi msanii na mtayarishaji wa muziki nchini Jetman hundi ya shilingi milioni 15 kutokana na michango iliyotolewa na watu mbalimbali kwaajili ya matibabu yake.
Michango hiyo imekusanywa kutokana na kampeni iliyoanzishwa na kituo hicho iliyopewa jina la Amka na Jetman.
Wakati huo huo mbunge wa jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula amechangia kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya matibabu hayo. Kiasi cha takribani milioni 20 kimekusanywa katika kampeni hiyo.
Jetman amekuwa kitandani kwa takriban miaka mitano kutokana na tatizo la kupooza mgongo.
Post a Comment