Timu ya Alikiba ilikata tiketi za ndege kwa awamu mbili kwaajili ya rapper M.I Abaga kusafiri kutoka Nigeria kwenda Afrika Kusini ili kuungana na staa huyo kushoot video ya wimbo aliomshirikisha, Aje.
Hata hivyo pamoja na hivyo, M.I hakuweza kutokea na hivyo ikamlazimu Alikiba kushoot kwa mara nyingine video bila kuwa na rapper huyo na CEO wa label ya Chocolate City.
Akiongea kwenye dinner maalum iliyoandaliwa kwenye hoteli ya Double Tree jijini Dar baada ya mapokezi yake ya Jumanne hii, Kiba alisema M.I alionesha kuwa ni mtu anayejali zaidi biashara zake.
“Hatukutaka kuingilia ratiba zake kwahiyo sisi tuliweza kufanya ile ya Kifaransa tukamaliza video. Lakini hii ya sasa hivi vile vile tulijitahidi kwa nguvu zetu zote kuhakikisha M.I atakuwepo lakini kuna sababu ambazo sisi wenyewe, management yangu ziko nje ya uwezo wetu,” alisema Kiba.
“Sababu tuliweza kukata tiketi mara mbili, namaanisha siku mbili tofauti, licha ya kutumiwa tiketi kwa mara ya kwanza bahati mbaya akakosa ndege na siku ya pili tena ikakosekana ndege. Kwahiyo kibinadamu tu haipendezi, sio kwamba kuonesha tuna hela ama nini kwamba tumtumie tena tiketi ya tatu, tukaona haina shida, we can do this,” aliongeza.
Alikiba amesema hiyo ndio sababu aliamua kuifanya video ya Aje Remix kwa utofauti zaidi ili kuziba pengo hilo.
Post a Comment