RC Makonda kuja na awamu ya pili ya majina ya watuhumiwa wa Madawa ya kulevya?
Baada ya jeshi la Polisi jana kutangaza kuwa awamu ya kwanza ya mapambano dhidi ya biashara ya Madawa ya kulevya kuleta matunda baada ya kupatikana kwa watuhumiwa 112 pamoja na kete 299 za Madawa ya kulevya, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye ndiye kinara wa mapambano yao atema cheche mtandaoni.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro akiwa ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.
Ikiwa bado wadau mbalimbali wakiendelea kujadili namna ambayo inatumiwa na mkuu huyo ya kuwataja watuhumiwa hadharani, RC huyo amepost picha akiwa na Simon Sirro na kuandika ujumbe ambao unaonyesha wajipanga kuja na list mpya.
“Maandalizi ya awamu ya pili yamekamilika,” aliandika RC Makonda Instagram.
Kauli hiyo imewafanya mashabiki katika mitandao ya kijamii kutafsiri kuwa mkuu huyo anakuja na list mpya ya watuhumiwa wa Madawa ya kulevya.
Jeshi hilo Jumatatu hii lilisema litawapandisha mahakamani watuhumiwa 12 huku wengine 100 wakiendelea kushikiliwa kwajili ya kukamilisha upelelezi.
Post a Comment