Radio na Weasel kumshirikisha Snoop Dogg kwenye remix ya ‘Plenty Plenty’
Kwa sasa wasanii wa Afrika wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kuhakikisha muziki wao unafika nchini Marekani ambao ndio sehemu ngumu sana kupenya. Radio na Weasel wanaounda kundi la pamoja ni miongoni mwa wasanii wa Afrika wanaolisaka tobo hilo.
Mastaa ho kutoka Uganda tayari wameshafanya kolabo na rapper Snoop Dogg kwenye remix ya wimbo wao ‘Plenty Plenty’ ambao wameuachia takriban miezi mitatu iliyopita.
Kupitia akaunti ya mtandao wa Instagram ya wasanii hao, wamethibitisha kufanyika kwa kolabo hiyo kwa kuandika, “Shhhh Let The Music Speak #PlentyPlenty Remix Dropping soon. Blessup @bet_africa @snooplion@snoopdogg @thulilegama.”
Huo utakuwa wimbo wa kwanza kwa wasanii wa Uganda kumshirikisha msanii mkubwa wa Marekani.
Post a Comment