Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Dogo Janja asema mwonekano wa mavazi ni kitu anachokizingatia zaidi kwenye muziki wake
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Tip Top Connection Dogo Janja amefunguka kwa kusema kuwa anaamini mwonekano wa msanii ni kit...


Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Tip Top Connection Dogo Janja amefunguka kwa kusema kuwa anaamini mwonekano wa msanii ni kitu cha msingi katika kumkuza msanii pamoja na brand yake.

Dogo Janja akiwa ametupia nguo za aina tofauti tofauti
Rapper huyo toka avunje ukimya na kuingia tena kwenye muziki amekuja kitofauti katika mwoneano ya mavazi pamoja na style za nywele zake.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Dogo Janja amedai yeye anaamini brand ya msanii inaanza kuonekana katika mwonekano wa mavazi.
“Nashukuru sana kama watu wamenza kuniona kwa jicho la tofauti katika mwonekano wangu, mimi naamini mavazi au mwonekano wa msanii katika mavazi ni kitu ambao kinaikuza brand pamoja na kuonekana tofauti na wasanii wengine,”alisema Dogo Janja.
“Kwa hiyo naweza kusema kwangu mimi ni kitu ambacho nakizingatia sana katika muziki wangu, tena na team yangu kabisa ambayo inaniangalia kabisa, hapa umechemka, hapa fanya hivi lakini yote ni kumtafuta Dogo Janja ambaye anamwonekano tofauti na wakuvutia,” aliongeza.
Kwa sasa rapper huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Kidele, anajipanga kuachia kazi mpya hivi karibuni ambayo amedai itakuwa tofauti kabisa na kazi ambazo amewahi kuzifanya.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top