Watu 39 wauawa siku ya mwaka mpya kwenye klabu ya usiku Instabul
Mtu aliyekuwa na bunduki aliwafyatulia risasi watu waliokuwa wakisherehekea mwaka mpya kwenye klabu ya usiku mjini Istanbul, Uturuki na kuua 39, Jumapili. Miongoni mwa waliopoteza maisha wamo raia wengi wa kigeni.
Ndugu
wakiwa kwenye mazishi ya Ayhan Arik, mhanga wa tukio la mauaji kwenye
klabu ya usiku ya Reina, Istanbul, Ururuki, January 1, 2017.
REUTERS/Osman Orsal
Kusudi la shambulio hilo bado halijabainika lakini kuna uwezekano likawa limefanywa na kundi la Islamic State ambalo limehusishwa na matukio mengi ya kigaidi nchini humo mwaka jana.
Polisi wanaendelea kumsaka muuaji huyo.
Post a Comment