WANAFUNZI WA TUDARCo WATOA MSAADA HOSPTALI YA PALESTINA
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Tumaini mwaka wa tatu wakiwa katika picha ya pamoja chuoni hapo.
Afisa Mhuguzi wa Hospitali ya Sinza Palestina, Aliho Ngerageza (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa wanafunzi wa Shahada ya Mawasiliano ya Umma mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Tumaini Tawi la Dar es Salaam (Tudarco), kwa ajili ya wanawake na watoto waliolazwa hospitalini hapo anaekabidhi ni Enock Bwigane na katikati ni Mhadhiri wa somo hilo chuoni hapo, Mary Kafyome
Mhadhiri wa somo la Public Relations chuoni hapo, Mary Kafyome akizungumza na vyombo vya habari.
Mhadhiri
wa somo la Public Relations chuoni hapo, Mary Kafyome akitoa msaada kwa
mgonjwa aliyelazwa hosptalini hapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Wanaochangia damu wa kwanza kushoto ni Marietha Tairo na Ole Kimosa,aliyesimama ni nesi akisaidia kufanikisha zoezi hilo.
Mhadhiri wa somo la Public Relations chuoni hapo, Mary Kafyome wa kushoto akiwa na Sara wakiendelea na kufanya usafi.
Baadhi wa wanafunzi wakifanya usafi katika Hosptali ya Palestina.
Wanafunzi
wa mwaka wa tatu wanaosoma Shahada ya Mawasiliano ya Umma, katika Chuo
Kikuu cha Tumaini (TUDARCo), kwa udhamini wa Mfuko wa Bima ya Afya
(NHIF), jijini Dar es Salaam.
wametembelea
hospitali ya Sinza (Palestina) na kutoa msaada wa vitu mbali
mbali,pamoja na kuchangia damu ili kusaidia kuokoa wajawazito na
majeruhi wanaofika hosptali hapo kupatiwa matibabu na kujifungua.
Mbali
na msaada huo wa vifaa vya watoto vikiwamo maji, juisi, nepi na vifaa
vya usafi, wanafunzi hao pia walijitolea kuchangia damu ikiwa ni sehemu
ya kusaidia na kujenga mahusiano mema na jamii inayowazunguka katika
somo la Mahusiano ya Umma (Public Relations).
Muuguzi
Gerangeza alisema hospitali yake imefurahi kupokea msaada huo hasa damu
kwani hospitali ina upungufu wa damu kutokana na kupokea wagonjwa wengi
wenye uhitaji wa damu.
“Mahitaji
ya damu ni makubwa kwa siku tunatumia uniti sita hadi 10, kwani kwa
siku tunapokea wajawazito 30 hadi 35 ambao wanahitaji damu, wakati
mwingine huwa tunaazima Hospitali ya Amana au Mwananyamala.
“Kwa
hiyo tunawashukuru sana kwani damu haipatikani dukani isipokua kwa
wasamaria kama ninyi naomba na vyuo vingine na taasisi waige mfano
wenu,” alisema Gerangeza.
Mwalimu
wa somo la Mahusiano ya Umma, aliyeambatana na wanafunzi hao, Mary
Kafyome alisema licha ya zoezi hilo kuwa ni sehemu ya somo lakini pia ni
kuunga mkono juhudi za serikali za kufanya usafi katika maeneo
yanayowazunguka.
“Rais
anahamasisha usafi tukaona ni vyema nasi mbali na kutoa msaada tumuunge
mkono. Lakini pia kupunguza vifo vya wajawazito na watoto kwa sababu ya
kukosa damu.
“Pia
naomba nitoe wito kwa vyuo vikuu, tuhakikishe tunawajenga wanafunzi
wetu kwa vitendo si kufundisha darasani pekee, naamini watakuwa mabalozi
wazuri wa vyuo vyetu katika taasisi watakazoenda kufanyia kazi katika
kusaidia jamii hata kwa faida ndogo waliyoipata,” alisema Kafyome.
Baadhi
ya wanafunzi walisema wamefurahia zoezi hilo kwani linawajenga kuwa
maofisa uhusiano bora katika taasisi na kampuni watakazofanyia kazi.
Post a Comment