Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: MKUU WA WILAYA YA MKURANGA FILBERTO SANGA AFUNGUA RASMI LIGI YA MBUNGE (ULEGA CUP)
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
MKUU WA WILAYA YA MKURANGA FILBERTO SANGA AFUNGUA RASMI LIGI YA MBUNGE (ULEGA CUP) LIGI ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga  (Ulega Cup) i...

MKUU WA WILAYA YA MKURANGA FILBERTO SANGA AFUNGUA RASMI LIGI YA MBUNGE (ULEGA CUP)


LIGI ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga  (Ulega Cup) imefunguliwa  rasmi jana kwa kuzikutanisha timu za Kipalang'anda  kombaini Fc na Mkuranga kombaini uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga.

Mashindano  hayo yamefunguliwa  na mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga  ukishuhudiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Juma Abed pamoja na baadhi ya madiwani wanaounda halmashauri hiyo.

Michuano hiyo ambayo ilianzia ngazi ya Vijiji ilishirikisha timu  125 na  baadae kuchujwa na kubakia timu 25 ambazo zimeingia ngazi ya wilaya na mshindi wa ligi hiyo ndio atakuwa bingwa wa wilaya. 

Akizungumza  na wachezaji wa timu hizo katika ufunguzi wa michuano hiyo Mkuu wa Wilaya hiyo Firbato Sanga  alisema michezo ni udugu na ujirani mwema hivyo aliwatakia michezo mwema.

Akizungumzia michuano hiyo Mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega amesema kuwa ni matarajio yake michuano hiyo itakwenda vyema  na lengo lake kubwa nikuona wanapata vijana wenye vipaji na watakaoweza kuipaisha Mkuranga.

"Nimatarajio yangu mambo yatakwenda kama nilivyopanga na kama mnavyoona wenyewe waandishi wa habari  vijana wa kutoka Mkuranga ndio wanaocheza "alisema Ulega

Amesema  tangu awali alisha kataa timu hizo kukodi watu Kutoka nje ya Mkuranga na anashukuru Mungu hayo yamezingatiwa na katika michuano hiyo mshindi ndio atakuwa bingwa wa Wilaya.

Amesema kuwa ana matumaini makubwa kwamba kupitia ligi hiyo watapatikanika vijana wenye uwezo ambao wataweza kuchukuliwa  na timu kubwa.

Aidha amesema kuwa michezo ni Afya ,ajira,na upendo kwani kupitia mashindano hayo watakuwa wametengeneza ujirani mwema hivyo watumie fursa hiyo kudumisha Umoja na mshikamono miongoni mwao.

Mchezo huo ulimalizika kwa goli moja lililofungwa na mchezaji wa timu ya Mkuranga Kombaini,Abdallah Mohamed  katika dakika ya kumi kipindi cha kwanza.

 Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ufunguzi wa Ligi ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga  (Ulega Cup)  uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga akizungumza  na wachezaji wa timu  za Kipalang'anda  kombaini Fc na Mkuranga kombaini katika ufunguzi wa Ligi ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga  (Ulega Cup)  uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Juma Abed  katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Mkuranga Kombaini pamoja viongozi mblimbali katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kipalang'anda  kombaini Fc katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani. 
 .Sehemu ya mashabi wa timu ya  Kipalang'anda  kombaini Fc na Mkuranga kombaini wakiwa wakishuhudia mtanange  katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani
.Mchezo ukiendelea ambapo mchezo huo ulimalizika kwa goli moja lililofungwa na mchezaji wa timu ya   Mkuranga Kombaini,Abdallah Mohamed katika dakika ya kumi kipindi cha kwanza.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top