WACHINA WASHEHEREKEA MWAKA MPYA WAO KATIKA VIWANJA VYA MNZI MMOJA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema
kuwa Tanzania itaendelea kudumisha,kuimarisha na kuendeleza mahusiano
mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na China kwa ajili ya manufaa ya
wananchi wa pande hizo mbili.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika viwanja vya Mnazi
Mmoja Jijini Dar es Salaam katika sherehe ya maadhimisho ya mwaka mpya
wa Kichina hapa nchini sherehe ambazo zimehudhuriwa na mamia ya raia wa
China na Tanzania.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa China imekuwa mshirika na
mdau mkubwa wa maendeleo hapa nchini na hali hiyo inatokana na mahusiano
mema na mazuri yaliyopo kati ya nchi hizi Mbili.
Makamu
wa Rais amemhakikishia Balozi wa China hapa nchini Dkt Lu Youqing kuwa
serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli itakuwa bega kwa bega na serikali ya
China hasa katika uimarishaji wa sekta za biashara, utamaduni, elimu,
afya na masuala ya kijeshi kwa ajili ya maslahi na ustawi wa wananchi
wa Tanzania na China.
Makamu
wa Rais amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kujifunza mambo mengi
kutoka China ili kuharakisha shughuli za maendeleo za wananchi kutokana
na Taifa la China kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo.
Amehimiza
ubadilishanaji wa wataalamu kati ya Tanzania na China katika sekta
mbalimbali kama hatua ya kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi nchini.
Kwa Upande wake,
Balozi wa China hapa nchini Dkt Lu Youqing amepongeza hatua
zinachukuliwa na serikali ya Tanzania katika kupambana na rushwa na
ufisadi.
Dkt
Lu Youqing amesema serikali ya China na raia wake wanafurahishwa na
hatua hizo kwa sababu zinalenga kuondoa na kukomesha rushwa na ufisadi
kwani tabia hizo zikiachwa ziendelee zinachangia kwa kiasi kikubwa
kuzorotesha utoaji wa huduma bora na za msingi kwa wananchi.
Akizungumzia
mwaka mpya wa Kichina hapa nchini Balozi huyo amesema maadhimisho hayo
ni muhimu kwa sababu raia Wachina na Tanzania wanajumuika pamoja katika
kubadilisha mawazo na kutakiana heri na mafanikio kwa mwaka 2017.
Balozi
huyo wa Tanzania hapa nchini Dkt Lu Youqing pia amewashukuru wananchi
wa Tanzania kwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mnazi Moja
katika kusheherekea sikukuu ya Mwaka mpya wa Kichina sherehe ambazo
inapambwa na michezo mbalimbali ikiwemo sarakasi na vikundi vya ngoma
asili kutoka China na maonyesho.
Katika
Maadhimisho hayo, Balozi wa China nchini Tanzania Dkt Lu Youqing
amemkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mfano wa hundi ya
shilingi milioni 70 fedha ambazo zitatumika katika ujenzi kwenye shule
ya msingi Chato iliyopo mkoani Geita.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa Jamhuri ya
Watu wa China zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipokea hundi ya shilingi milioni 70 kutoka kwa Balozi wa China nchini
Mhe. Dk. Lu Youqing iliyotolewa na Taasisi pamoja na Jumuiya ya Wachina
wanaoishi Tanzania kuchangia shule ya msingi ya Chato iliyopo mkoani
Geita wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa kichina
zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni wengine waalikwa pamoja na
wasanii waliotumbuiza wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa
kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam.
Sehemuya watu waliohudhuria sherehe za mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Balozi wa China nchini Mhe. Dk. Lu Youqing wakati wa
maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Post a Comment