KIKAO CHA KUTAFUTA SULUHU YA MGOGORO WA PORI TENGEFU LA LOLIONDO CHAENDELEA CHINI YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA ,MRISHO GAMBO
Mkuu
wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo ameendelea kuongoza vikao vya kutafuta
suluhu ya mgogoro wa Pori Tengefu ambao umechukua muda mrefu.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa katika zaiara yake mwezi desemba mwaka jana
alimwagiza Mkuu mkoa kuwakutanisha wadau wote na kupata maoni yao ili
kuumaliza kabisa mgogoro huo.
Katika
kipindi cha siku saba wajumbe wamekutana na kujadili chanzo na hatua
zilizochukuliwa pia wametembelea eneo lilikusudiwa kutengwa kwaajili ya
mapito ya wanyama na mazalia ya nyumbu sanjari na kuangalia vyanzo vya
maji na miundombinu.
Gambo
amesema serikali iko makini kuangalia njia bora za uhifadhi huku
wananchi wakiendelea na maisha yao ya ufugaji bila kuathiri sekta ya
utalii kwa ujumla huku maslahi ya wawekezaji yakilindwa kwani wana
mchango mkubwa katika kusukuma mbele maendeleo ya taifa yanayotokana na
kodi wanazolipa.
Taasisi mbalimbali zimewakilishwa zikiwemo Tanapa,NCAA,Tawiri,Asasi za kiraia,Jamii ya wananchi wanaoishi Loliondo na serikali ya mkoa na wilaya.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uratibu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Ardhi,Jason Kami akiwasilisha mpango wa matumizi ya ardhi katika Pori Tengefu la Loliondo. |
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uratibu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Ardhi,Jason Kami akiwasilisha mpango wa matumizi ya ardhi katika Pori Tengefu la Loliondo. |
Kaimu Mkurugenzi Wanyamapori nchini,Profesa Alexander
Songorwa akizungumza umuhimu wa uhifadhi na kutenga eneo la ukubwa wa kilometa
za mraba 1,500 kwaajili ya mapito na mazalia ya wanyama.
|
Wadau kutoka taasisi mbalimbali wakisikiliza kwa makini
mawasilisho ya makundi mbalimbali katika kikao cha kutafuta suluhu ya mgogoro
wa Pori Tengefu la Loliondo.
|
Wadau kutoka taasisi mbalimbali wakisikiliza kwa makini mawasilisho ya makundi mbalimbali katika kikao cha kutafuta suluhu ya mgogoro wa Pori Tengefu la Loliondo. |
Diwani wa Kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro akiwasilisha maoni ya wenyeji na kuomba serikali iache mpango wake wa kulichukua eneo hilo kwani jamii inalihitaji. |
Post a Comment