Rais wa Korea Kusini agoma kuhudhuria mahakamani siku ya kwanza ya kesi yake
Rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye ameshindwa kuhudhuria katika mahakama ya kikatiba ya nchi hiyo Jumanne hii kusikiliza kesi yake inayomkabili kuhusu ufisadi na kutumia vibaya madaraka.
Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa na majaji tisa ambao wamehairisha kusikiliza kesi hiyo mpaka Alhamisi hii. Wakati huo huo wakili wa Rais Geun-hye, Lee Jung-hwan amedai kuwa mteja wake hataweza kuhudhuria siku hiyo.
Mahakama hiyo imesema kuwa haitamlazimisha Rais huyo kuhudhuria kusikiliza kesi hiyo lakini endapo mara ya pili asipokuwepo kesi hiyo itaendelea bila ya yeye kuwepo.
Majaji hao wana siku 180 kuamua iwapo Rais Park ambaye amesimamishwa kazi anafaa kuendelea kuiongoza nchi hiyo au kuondoka madarakani kwa kuwa bunge lilishamaliza kupiga kura ya kumpinga kuiongoza nchi hiyo tangu mwezi uliopita.
Post a Comment