Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Prince Harry adai aliipenda Afrika baada ya mama yake, Princess Diana kufariki
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Prince Harry adai aliipenda Afrika baada ya mama yake, Princess Diana kufariki Prince Harry amesema aliipenda sana Afrika baada ya b...

Prince Harry adai aliipenda Afrika baada ya mama yake, Princess Diana kufariki


Prince Harry amesema aliipenda sana Afrika baada ya baba yake Prince Charles, kumleta kukwepa vurugu zilizofuata baada ya kifo cha mama yake, Princess Diana.

Harry ameliambia jarida la Town & Country toleo la February lenye ripoti ya kazi yake inayohusiana na kuwalinda tembo waliopo hatarini barani Afrika.
“Nilikuja mara ya kwanza mwaka 1997, moja kwa moja baada ya mama yangu kufariki. Baba yangu alimuambia kaka yangu na mimi kufunga mizigo – tunaenda Afrika kuwa mbali na yote.”
Aliongeza, “Hii ndio sehemu ambayo huwa najisikia zaidi kama mimi kuliko sehemu yoyote duniani. Natamani ningetumia muda mwingi Afrika. Nina hii hisia kubwa ya pumziko lililokamilika na ukawaida hapa.”

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top