Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Picha: Ali Hassan Mwinyi awataka waislamu kuyaenzi mema ya Mtume Muhammad (S.A.W)
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Picha: Ali Hassan Mwinyi awataka waislamu kuyaenzi mema ya Mtume Muhammad (S.A.W) Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muunga...

Picha: Ali Hassan Mwinyi awataka waislamu kuyaenzi mema ya Mtume Muhammad (S.A.W)


Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Al-Haji Ali Hassan Mwinyi amewataka watanzania kuwa na tabia ya kuyafanyia muendelezo yale mema yaliyofanywa na Mtume Muhammad (S.A.W).

Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Al-Haji Ali Hassan Mwinyi akikaribishwa katika maulidi hayo yaliyoandaiwa na kampuni ya Nida Textile Mills.
Akiwa katika hafla hiyo ya Maulidi iliyofanyika jijini Dar es Salaam Al-Haji Mwinyi ameeleza kuwa Mtume Muhammad alikuwa akifunga kila siku ya Jumatatu ikiwa ni ishara ya kusherekea siku aliyozaliwa hivyo ni vyema kuiga mfano huo wa kufanya matendo mema kwa kuyarudia mara kwa mara na kuyadumisha, huku akipongeza uongozi wa NIDA kwa kuwaalika na kusherekea pamoja kwani amejifunza mengi kupitia mawaidha yaliyotolewa na viongozi wa dini waliohutubia akiwemo Sheikh Ally Basaleh.
Sherehe hizo zimepambwa kwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali akiwemo Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Gharib Bilal, Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo, Naibu Waziri Wizara ya Afya Hamis Kigwangala, Waziri wa zamani wa Ulinzi Profesa Juma Kapuya, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba, Mbunge wa Mkuranga Juma Ulega huku kwa viongozi wa dini walikuwepo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum na Kadhi Mkuu wa Tanzania Abdallah Mnyaa ambapo wote kwa pamoja walipewa zawadi maalum na kampuni hiyo.

Profesa Lipumba akiwasili katika eneo la maulidi

Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo, na Naibu Waziri Wizara ya Afya Hamis Kigwangala wakikaribishwa

Waislamu waliojitokeza kwenye maulidi hayo


















About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top