Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Karrueche awagombanisha Chris Brown na Soulja Boy
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Karrueche awagombanisha Chris Brown na Soulja Boy Mwaka 2017 umeanza vibaya kwa Chris Brown na Soulja Boy – kwakuwa wameanzisha bifu chan...

Karrueche awagombanisha Chris Brown na Soulja Boy


Mwaka 2017 umeanza vibaya kwa Chris Brown na Soulja Boy – kwakuwa wameanzisha bifu chanzo kikiwa ni mrembo Karrueche Tran.

Tangu alipoachana na Karrueche Chris amekuwa akimfuatilia mrembo huyo huku mara kadhaa akigombana na wanaume ambao wanaomtolea udenda. Na sasa balaa limemkumba rapper Soulja Boy baada ya kulike picha ya mrembo huyo kwenye mtandao wa Instagram kitendo ambacho kimeonekana kumkera Brown.
Soulja Boy amefunguka kupitia mtandao wa Twitter kuwa Chris amemtafuta na kumpiga mikwara baada ya kulike picha hiyo.



Chris Brown amekuwa akijaribu mara kadhaa kutaka kurudiana na Karrueche lakini imekuwa ngumu kwa mrembo huyo kukubali.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top