George Michael aongoza chati za muziki baada ya kifo chake
Hakuna kinachompa kiki mwanamuziki zaidi ya kifo chake!
Katika wiki moja tangu kifo cha George Michael, muimbaji huyo amerejea kwenye chati za albamu bora 10 kwa mara ya kwanza tangu miaka 17 iliyopita.
Album yenye mkusanyiko wa nyimbo zake zilizotamba, ‘Ladies & Gentlemen,’ imeongezeka mauzo kwa zaidi ya asilimia 5,625 katika siku 7 zilizopita na kumfanya akamate nafasi ya 8 kwenye chati.
Wakati huo huo, imedaiwa kuwa muimbaji huyo atapewa heshima za mwisho mara mbili – kwa marafiki na familia pamoja na mashabiki, kwa mujibu wa The Mirror. Pia rafiki yake Sir Elton John atatumbuiza kwenye moja ya sherehe hizo.
Michael alifariki siku ya Christmas akiwa na miaka 53.
Post a Comment