Fid Q asema yupo tayari kufanya kolabo na Nay wa Mitego
Msanii wa muziki wa hip hop, Fareed Kubanda aka Fid Q amedai yupo tayari kufanya kolabo na rapper Nay wa Mitego kwa kuwa ni mmoja kati ya wasanii wa hip hip ambao wanafanya vizuri.
Alisema hayo baada ya hivi karibuni kupitia kipindi cha Planet Bongo ya EA Radio, Nay wa Mitego amemtaja Fid Q kuwa miongoni mwa rappers anaowakubali zaidi Bongo na kusema kuwa hastahili kufananishwa naye sababu yeye ni rapper mwepesi.
Ijumaa hii akiwa katika kipindi cha Enewz cha EATV, Fid Q amedai yeye anaufuatilia muziki wa Nay wa Mitego huku akidai yupo tayari kufanya naye kolabo.
“Nimeipenda sana ngoma ya Nay wa Mitego ‘Sijiwezi’ hasa ile chorus, na niko tayari kufanya naye kolabo,” alisema rapper huyo.
Rapper huyo ambaye ameachia wimbo ‘Kemosabe’ hivi karibuni, amedai Nay wa Mitego siyo rapper mwepesi kama anavyojiona kwani ni mmoja kati ya marappers wenye uwezo mkubwa.
Post a Comment