Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza jambo wakati wa mkutano wa
kujadili matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo. Kushoto ni wajumbe wa
Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Tegeruka, Musoma Vijijini
waliohudhuria mkutano wa kujadili matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo
hilo.
Katibu wa Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini na Afisa Mipango wa
Wilaya ya Musoma, Mukama Rugina (aliyesimama) akizungumza wakati wa
mkutano wa kujadili matumizi ya fedha za mfuko huo.
Diwani wa Kata ya Tegeruka, Benjamin Maheke (aliyesimama)
akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili matumizi ya fedha za mfuko wa
Jimbo la Musoma Vijijini.
Wajumbe
wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini wameagizwa kuhakikisha
wanakagua utekelezaji wa miradi ya kilimo ya vikundi vilivyokabidhiwa
vifaa kutoka kwenye mfuko huo ili kujiridhisha.
Agizo
hilo limetolewa hivi karibuni na Mbunge wa Jimbo hilo, Profesa Sospeter
Muhongo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati husika wakati wa mkutano wa
hadhara wa kuainisha matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo kwa Awamu ya
Pili uliofanyika katika kijiji cha Tegeruka, Musoma Vijijini.
Ilielezwa
kwamba Awamu ya kwanza ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya Mfuko wa
Jimbo hilo ni shilingi milioni 70,820,000 ambazo zilitumika kwa matumizi
mbalimbali ikiwemo shilingi milioni 20,000,000 kwa ajili ya Kituo cha
Afya cha Murangi.
Fedha
zingine ni milioni 27,500,000 ambazo zilitumika kwa ajili ya kurekebisha
nyumba na madarasa yaliyokuwa yameezuliwa na upepo kwa shule mbili za
msingi, milioni 22,500,000 ilitumika kununulia mashine za umwagiliaji,
mbegu za mbogamboga na matunda pamoja na dawa za kilimo na shilingi
820,000 zilitengwa kwa ajili ya kuwezesha ufuatiliaji.
Profesa
Muhongo alisema ni jukumu la Kamati husika kuhakikisha fedha imetumika
kwa matumizi yaliyokubaliwa na aliagiza vikundi vyenye miradi ya kilimo
ambayo haijaanza vinyang’anywe vifaa vilivyokabidhiwa na vipewe vikundi
vingine vyenye vyenye nia dhabiti ya kuendeleza kilomo.
“Tembeleeni
hivi vikundi, mkikuta havijaanza kutumia vifaa tulivyowapatia
mvinyanga’anye na vifaa hivyo vigawiwe kwenye vikundi vyenye nia ya
dhati,” aliagiza Profesa Muhongo.Akizungumzia
Awamu ya Pili ya Mfuko wa Jimbo, Profesa Muhongo alisema Mfuko wa Jimbo
umepokea kiasi cha shilingi milioni 38,479,000 ambazo alisema Kamati
husika kwa kushirikiana na wananchi pamoja na madiwani wamependekeza
zitumike kwa ajili ya kuboresha kilimo.
Alisema
shilingi milioni 16,000,000 zitatumika kwa ajili ya kununulia mbegu za
kisasa za mihogo za mkombozi kiasi cha vipando 532,000 ambazo zitagawiwa
kwenye Kata 21 kwa ajili ya vijiji 68, na shilingi milioni 21,900,000
itatumika kununulia mashine 21 za kukamulia alizeti.
Aliongeza
kuwa hapo awali alisambaza mbegu za alizeti za majaribio kiasi cha kilo
4000 ambazo alisema zimeonesha mafanikio na hivyo aliongeza mbegu
zilizoboreshwa kutoka Arusha kiasi cha kilo 5000 ambazo pia
zilisambazwa.
Alisema
ili kujiongezea kipato kutokana na kilimo cha alizeti, wameamua badala
ya kuuza mbegu, wakulima hao watauza mafuta na ndiyo sababu ya kutenga
kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya mashine hizo ambazo alizielezea kuwa
ni za kuzungusha kwa mikono na hazihitaji mafuta wala umeme.
“Hizi nilitoa fedha yangu na sio katika mfuko wa jimbo; na kukitokea mapungufu nifahamisheni nijazilizie,” alisema.Akizungumzia
utaratibu wa mashine hizo, alisema kila Kata itakabidhiwa mashine yake
na kwamba zitafungwa kwenye ofisi za kata chini ya usimamizi wa Afisa
kilimo.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Related Posts
- Zanzibar to Organize a Half Marathon race to Promote Gender Mainstreaming, Attain Sustainable Development Goal06 Jan 20180
More than 300 Zanzibari women, men, girls and boys are expected to participate in t...Read more »
- Embassy of Kuwait in Tanzania Committed to Support Educational Projects in Zanzibar18 Dec 20170
Member of the House of Representative in Zanzibar, Hon Simai Mohammed Said in discussion ...Read more »
- Turkey to intensify relationship with SUZA16 Aug 20170
Delegation of Presidency for Turks Abroad and Related Communities (YTB) meets Prof. Rai (...Read more »
- RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH WATEMBELEA KUWAJULIA HALI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM28 May 20170
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamo...Read more »
- Halmashauri kunufaika na Tsh 250 bilioni za mradi wa maji vijijini18 May 20170
Halmashauri za wilaya zimetakiwa kuongeza ufanisi katika kusimamia miradi ya maji kwa kucha...Read more »
- NAIBU MKURUGENZI WA IMF AKUNWA NA UKUAJI WA UCHUMI WA TANZANIA, AAHIDI KUFUNGUA DIRISHA LA MIKOPO KWA TANZANIA18 May 20170
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kulia) akiel...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.