MGONJWA ASHINDWA KUPATA HUDUMA MUHIMBILI KWA KUWA NA UREFU USIO WA KAWAIDA
Kijana Baraka Elias Mashauri mwenye umri
wa miaka 35 mkazi wa Musoma mkoani Mara ameshindwa kupata matibabu
katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kutokana na urefu wake usio wa
kawaida.
Baraka anayesumbuliwa na tatizo ya nyonga ana kimo kirefu cha zaidi ya
futi 7 na hii kufanya kushindwa kupatiwa matibabu kufuatia vifaa katika
taasisi hiyo ikiwemo mashine za X- ray vitanda vya kufanyia upasuaji
kuwa vifupi ukilinganisha na urefu wake.
Tatizo hilo la nyonga linalomsumbua Baraka limemfanya ashindwe kutembea
na kulazimika kutumia magongo ambayo anasema yanamtesa kutokana na urefu
alionao.
Akizingumzia jinsi watu wanavyomshangaa kutokana na urefu wake alisema
kuwa kwake anaona fahari kwani ni maisha ambayo ameyazoea kila
anapokwenda. Amesema kuwa hiyo haimpi shinda kwani anajua wanamshangaa
kutokana na urefu wake kitu ambacho si kibaya.
Kuhusu ugonjwa unaomsumbua na baada ya kushindikana kupatiwa matibabu
nchini, Baraka ameomba wasamaria wema waweze kumsaida ili apatiwe
matibabu nje ya nchi ili arudie kwenye hali yake ya kawaida kwani
magongo anayotumia kutembelea yanamtesa.


Post a Comment