KAMBI YA UPINZANI YAUKUBALI MUSWADA WA HABARI KWA KUWEKA BIMA YA AFYA KWA WANAHABARI
Kambi
Rasmi ya upinzani Bungeni yaikubali Bodi ya Ithibati, Baraza Huru la
Habari pamoja na Bima ya Afya kwa waandishi wa habari nchini.
Akiwasilisha
maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni mjini Dodoma, Msemaji Mkuu wa
Kambi hiyo katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Joseph
Mbilinyi amesema kuwa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016
unamaufaa kwa wanahabari nchini
“Kifungu
cha 58 kinatoa jukumu na kuwataka waajiri wa waandishi wa
habarikuhakikisha kuwa waandishi wa habari wanakuwa na bima ya afya
pamoja na kuhakikisha kuwa wanachangia katika mifuko ya hifadhi za
jamii” alisema Mbilimnyi.Msemaji huyo aliendelea kusema “Jambo hili ni jema sana na Kambi Rasmi ya Upinzani inaliunga mkono”.
Kuanzishwa
kwa Bodi ya Ithibati pamoja na Baraza Huru la Habari ni jambo jema vitu
ambavyo vitalinda maslahi ya mwandishi wa habari kwa kuzingatia kuwa
moja ya kazi Baraza na Bodi ni kuweka viwango vya uangalizi pamoja na
utaratibu wa kitaaluma katika kuratibu tasnia ya habari nchini.
Mbilinyi
ametoa rai kwa Wabunge wote bila kujali itikadi za vyama kutambua kuwa
jukumu la kutunga sheria ni wajibu wao wa kikatiba ambayo wanawajibika
wakiwa sehemu ya Bunge kufanya kazi kwa maslahi mapana ya taifa.
Aidha,
Mbilinyi amesisitiza kuwa katika Mkutano wa Nne wa Bunge la 11 Septemba
15 mwaka huu, Serikali ilileta Muswada wa Huduma za Habari na kusomwa
mara ya kwanza kwa lengo la kuwapa nafasi Wabunge pamoja na wadau
mbalimbali wa habari kupitia na kuufanyia tafakuri ya kina na hatimaye
kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu Muswada huo.
Naye
Wiziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema kuwa
mageuzi katika tasnia ya habari nchini yataifanya kuwa taaluma kamili
itakayowaletea heshima wanahabari na taifa kwa ujumla.
Kupitishwa
kwa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari itatoa wigo mpana kwa
wanahabari kutekeleza majukumu yao kw uhuru ya kukusanya, kuhariri na
kuchapisha au kutangaza habari.
Waziri
Nape ameongeza kuwa pamoja na maboresho mengi ya Muswada huo pia
unzingatia suala la mitambo ya kuchapisha magazeti na majarida nalo
limepewa uzito unaostahili kwa kutohusika moja kwa moja kwa kosa la
gazeti ambalo limechapisha habari yenye makosa ya kisheria dhidi ya watu
au taasisi mbalimbali.
Akinukuu
maneno mbalimbali ya watu maarufu duniani juu ya masuala ya habari
akiwemo Rais wa Marekani Thomas Jefferson Januari 16, 1789, Rais wa
zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, Muasisi wa Taifa la India
Mahatma Ghandhi, Baba wa Uhuru wa Habari John Stuart Mill (1806-1873)
pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Waziri Nape alimesma
kuwa mmoja wa viongozi hao Mahatma Ghandhi aliamini kuwa uhuru wa kweli
wa kujieleza ni ule unaoweka mbele heshima ya watu wengine na kuwalinda
dhidi ya dhara, kebehi, kejeli na madhara mengine huku Baba wa Uhuru wa
Habari John Stuart Mill akibainisha dhima ya uhuru wa vyombo vya habari
na umuhimu wa kuwa huriu unapaswa kuzingatia ukomo wa haki ya kupata
habari kuwa unakoma pale haki za watu wengine zinapoanzia.
Akichangia
katika mjadala wa Muswada huo wakati, Mbunge Sixtus Mapunda amesema
kuwa kwa muda mrefu tasnia ya habari haikuwahi kupata hadhi inayostahili
ndani ya nchi pamoja na kazi nzuri ya kuhabarisha, kufundisha, kukosoa
na kuwasaidia watu watu wenye matatizo wenye changamoto mbalimbali hata
kufikia hadhi ya kuitwa muhimili wan ne wa dola.
“Tasnia
hii haikuwahi kulindwa, tasnia hii haikuwahi kuenziwa, tasnia hii
haikuwahi kuheshimiwa inayostahili, kwa mwandishi wa habari mwenyewe,
kwa chombo cha habari na wamiliki wa chombo cha habari tofauti na tasnia
nyingine nyingine, kwa mara ya kwanza ndani ya nchi hii, heshima ya
tasnia inapatikana” alisema Mapunda.
Mapunda
ameitaja tasni hizo kuwa ni za Madaktari, Wahasibu na Wahandisi ambao
wanachombo chao kinacholinda maslahi yao, maadili yao na kinachowalinda
ili kuendelea kulinda taaluma yao.
Aidha,
Mapunda amesema kuwa kwa miaka miaka zaidi ya 23, Muswada utasaidia
kutatua matatizo yote yaliyokuwa yanatokana na mapungufu ya Sheria ya
Magazeti ya mwaka 1976 kwa kuwa na Bodi ya Ithibati, Baraza Huru la
Habari, Bodi ya Ithibati Mfuko wa Mafunzo ambayo ni mambo mapya.
Zaidi
ya hayo, Mapunda aliongeza kuwa watu wenye vipaji vya kuandika habari
kulingana na taaluma zao ikiwemo uchumi hawajazuiliwa na Muswada wa
Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016.
Chimbuko
la Muswada huo linatokana na baadhi ya vipengele vya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania baada ya kufanyiwa marekebisho mwaka 1984 ambapo
haki ya kikatiba ya kutafuta, kupokea na kutoa habari imeainishwa
kwenye Ibara ya 18 (b) pamoja na mikataba mbalimbali ya kimataifa ya
inayoainisha haki na wajibu wa sekta ya habari.
Mkataba
huo wa Kimataifa ni ule wa Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966
ambao Tanzania iliuridhia Juni 11, 1984 pamoja na Mkataba wa Afrika wa
Haki za Binadamu na Watu 1981 ambao nao uliridhiwa Februari 18, 1984.


Post a Comment