Rapa Young Dee amefunguka mambo kadhaa kuhusu Young Killer na Dogo Janja kumchana mara kwa mara kwenye ngoma zao.
Young Dee amekiambia kipindi cha The Play List cha Times Fm kuwa
wasanii hao ni umri tu wanapitia kwa sasa ambao yeye ameshapita huko
hivyo hawashangai.
Kuhusu line ya Dogo Janja iliyopo katika wimbo wake wa ‘My Life’
isemayo, “nyie mayoung hamniwezi’, Young Dee alisema amekuwa akifuatilia
nyimbo kama hizo kwa muda mrefu na sio hiyo tu kuna nyimbo karibia sita
na nyingine zipo studio hazijatoka.
“Huu wimbo My Life maana yake maisha yangu, kama naimba wimbo
unaohusu maisha yangu siwezi kumzungumzia mtu mwingine, wimbo ni mzuri
lakini hiyo part imekuwa kama imetoka nje ya mada.
“Hata kama wewe ni mkali fanya mambo yako achana na mtu mwingine,
simple like that, siwezi kusema mimi ni mkali eti wewe Fid Q huniwezi,
hilo hamna kama wewe ni mkali fanya ukali wako,” alisema Young Dee na
kuongeza.
“Ni kama shambulio la moja kwa moja lakini huwezi kujua mtu anafanya
hiyo kwa lengo gani, mwingine anatafuta publicity, kwa hiyo mimi
nitavyoreact ndio itafanya hiyo point ionekane ina make sense au sivyo,”
alisema.
Pia aliuchambua line ya Young Killer katika wimbo wa Sinaga Swagga
isemayo, “kuhusu kufunikwa siwazi, kuhusu Janjaro na Young Dee mimi ndio
mkubwa wao wa kazi,”.
Kuhusu line hiyo Young Dee alisema anajua wanakuwa na itafika point
wataacha hayo mambo na kuamua kufanya kazi, lakini sasa hawajaamua
kufanya kazi bado wapo kwenye vilinge.
“Na mimi ninapenda kwa sababu wenye wanajua kabla hawajatoka mimi
ndiye nilikuwa nawapromote, huyo Young Killer nimempigia simu mimi
nikiwa na Belle 9 nakamuhamasisha baada ya kumsikia kwenye kipindi cha
Fid Friday Free Style.
“Dogo Janja kabla hajaingia Tip Top, pale Tongwe nilimwambia J
Murder.mchukue huyu dogo anachana sana. Lakini siwezi kuwajudge kwa
sababu ni umri wanaopitia ambao hata mimi nilipitia,” alisema Young Dee.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment