Rapa kutoka King Cash, Young Dee amefunguka kueleza kilichosababisha akaondoka katika label yake ya zamani, Millian Dollar Boys (MDB) iliyochini ya producer Max Rioba.
Rapa huyo ambaye ameachia video ya wimbo
wake mpya ‘Bongo Bahati Mbaya’ akiwa chini ya label hiyo mpya, ameiambia
Bongo5 kuwa aliachana na label hiyo baada ya kushindwa kukubaliana
baadhi ya mambo.
“Nikianza na watu ambao nilikuwa
nikifanya nao kazi ni watu ambao nilikuwa nafanya nao kazi kama
familia,” alisema Young Dee. “So lilivyokuja suala la kifamilia kuna
baadhi ya vitu havikwenda sawa ndipo ikaoneka kila mtu aanze kufanya
kazi mwenyewe bila kumtegemea mtu mwingine,”
Aliongeza, “Mimi suala la kufanya kazi na
Mr Ttouch ni suala la muda hata hapo awali tulikuwa tunafanya kazi kama
washkaji. Kwahiyo baada ya kuona tunaweza kufanya kazi pamoja,
akanikutanisha na uongozi wa King Cash, wakanisaini kama msanii wao wa
kwanza,”
Rapa huyo alisema yeye pamoja na Mr TTouch wapo chini ya King Cash.
Post a Comment