Ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya African Lyon umeifanya
ifikishe pointi 62 na kuifikia rekodi waliyoiweka msimu uliopita
walipomaliza ligi wakiwa na jumla ya pointi 62 baada ya kucheza mechi
30.
Msimu uliopita Simba ilimaliza ligi ikiwa na pointi 62 baada ya
kucheza mechi 30 na kushika nafasi ya tatu nyuma ya Azam ambao walikua
nafasi ya pili huku Yanga wakiwa ndio mabingwa wa VPL.
Simba imerejea katika nafasi ya kwanza ikiwa imeizidi Yanga kwa
pointi tatu lakini Yanga wenye pointi 59 wapo nyuma kwa michezo miwili,
Simba imeshacheza mechi 28 hadi sasa wakati Yanga tayari imecheza mechi
26.
Goli la Ibrahim Ajib dakika ya 37 kipindi cha kwanza na goli la
kujifunga la Hamad Waziri dakika 55 kipindi cha pili ndio yameipa Simba
ushindi, huku goli pekee la Lyon likifungwa na Omar Abdalla dakika 47+4
kipindi cha kwanza.
Ubingwa wa VPL bado upo wazi kwa Simba na Yanga kwa mechi zilizosalia
lakini Yanga wapo katika nafasi nzuri endapo watashinda mechi zao zote
(nne) zilizosalia kabla ligi haijamalizika.
Endapo Simba watashinda michezo yao miwili iliyosalia watafikisha
pointi 68 wakati Yanga wakishinda mechi zao zote watafikisha pointi 71.
Simba imefikia rekodi yao ya msimu uliopita
Title: Simba imefikia rekodi yao ya msimu uliopita
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya African Lyon umeifanya ifikishe pointi 62 na kuifikia rekodi waliyoiweka msimu uliopita walipomaliza ligi...
Post a Comment