Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: SHIRIKA LA WOTESAWA LAZIDI KUSAMBAZA ELIMU YA KUTETEA HAKI ZA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI.
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Mwanasheria na Msimamizi wa Mradi wa Uwezeshaji Shirikishi kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani nchini Tanzania, Jackline Ngallo, aki...



Mwanasheria na Msimamizi wa Mradi wa Uwezeshaji Shirikishi kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani nchini Tanzania, Jackline Ngallo, akiwasilisha mada kwenye semina kwa Viongozi wa serikali za mitaa kutoka wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza.

Semina hiyo ya siku tatu, kuanzia jana Mei 09 imewashirikisha Madiwani, Watendaji wa Kata, Maafisa Maendeleo na Ustawi wa Jamii, Wenyeviti wa Mitaa na dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi imelenga kuwajengea uwezo viongozi hao ili kusaidia kutetea na kulinda maslahi ya mtoto mfanyakazi wa nyumbani na kumuepusha na utumikishwaji wa kazi ngumu na maslahi duni.

Mwanasheria wa Shirika la WOTESAWA, Jackline Ngallo, akiwasilisha mada kwenye semina hiyo ambapo pia ameelezea juu ya umuhimu wa viongozi hao kuitambua Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 ambayo inakataza mtoto chini ya umri wa miaka 14 kuajiriwa huku wale walio juu ya umri huo wakipaswa kuajiriwa kufanya kazi zisizo hatarishi.

Aidha amekumbusha juu ya kuutambua Waraka wa Mishahara wa mwaka 2013 ambao unaelekeza kwamba mfanyakazi wa kazi za nyumbani anapaswa kulipwa kiwango cha chini cha mshahara ambacho ni shingili 150,000 iwapo mwajiri ni balozi ama mfanyabiashara mkubwa, elfu 80,000 ikiwa mwajiriwa haishi kwenye nyumba ya mwajiri wake, elfu 40,000 ikiwa mwajiriwa anaishi kwenye nyumba ya mwajiri wake na shilingi 130,000 ikiwa mwajiri ni rai wakigeni.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwasilisha maoni yao baada ya majadiliano katika makundi
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwasilisha maoni yao baada ya majadiliano katika makundi
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akichangia mada
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwasilisha maoni yao baada ya majadiliano katika makundi
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo
Semina hiyo ilianza jana Mei 09,2017 na inatamatika kesho Mei 11,2017 Jijini Mwanza

Waraka wa Mishahara wa mwaka 2013 kwa wafanyakazi wa nyumbani



Afisa kutoka shirika la WOTESAWA akiwa kwenye semina hiyo



Diwani wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza, John Kabadi, amesema semina hiyo itwasaidia katika kutetea maslahi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani ikiwemo kuwaepusha na utumikishwaji pamoja na ujira duni.



Gloria Shindika kutoka dawati la jinsia, kituo cha polisi Igogo Jijini Mwanza, amesema semina imewaongezea mbinu zaidi za namna ya kuwasaidia watoto wafanyakazi wa nyumbani watakaokuwa wakikumbwa na aina yoyote ya utumikishwaji.



Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyamanoro Kaskazini, Kata ya Ibungilo Manispaa ya Ilemela, ameeleza kutumia elimu aliyoipata kwenye semina hiyo katika kuwaelimisha wananchi wa mtaa wake katika kuhakikisha maslahi na haki za mtoto yanalindwa



Mwanasheria wa Shirika la WOTESAWA, Jackline Ngallo, akizungumza na Lake Fm Mwanza



Shirika la WOTESAWA linawahimiza wanajamii kwamba bado watoto wafanyakazi wa nyumbani wanayo haki ya kupata elimu hivyo ni vyema haki hiyo ikazingatiwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top