Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
amewasili mjini Arusha ambapo leo ataongoza wananchi wa mkoa wa Arusha
na mikoa ya jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32,walimu Wawili
pamoja na dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent iliyopo Jijini Arusha
waliopata ajali tarehe 06-May-2017 katika eneo la Rhotia wilayani Karatu
mkoani Arusha.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo pamoja na Viongozi wa wengine wa mkoa huo
Wanafunzi na walimu hao walipata ajali hiyo wakati wanaenda kwenye
shule iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mitihani wa ujirani mwema
baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia korongoni
kwenye eneo la Rhotia wilayani Karatu.
Ibada na dua za kuaga miili ya marehemu hao itafanyika katika uwanja
wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kuanzia Saa Mbili asubuhi hii leo.
Katika uwanja wa ndege wa Arusha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na ujumbe wake wamepokelewa na
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo pamoja na Viongozi wa wengine wa
mkoa huo.
Miili ya wanafunzi 32 kuagwa leo Arusha
Title: Miili ya wanafunzi 32 kuagwa leo Arusha
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Arusha ambapo leo ataongoza wananchi wa mkoa wa Arush...
Post a Comment