Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Emmanuel Macron ashinda kiti cha urais Ufaransa
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Taifa la Ufaransa Mei 8.2017, wameamua maamuzi magumu baada ya kumpigia kura za kishindo mgombe wa kiti cha Urais machachali na kijana mwe...
Taifa la Ufaransa Mei 8.2017, wameamua maamuzi magumu baada ya kumpigia kura za kishindo mgombe wa kiti cha Urais machachali na kijana mwenye umri mdogo wa miaka 39, Emmanuel Macron ambaye alipata asilimia 65.1 ya kura zake dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mwanamama Le Pen aliyepata ushindi wa asilimia 34.9.

Rais mteule wa Ufaransa, Emmanuel Macron
Awali wananchi wa Taifa hilo walijitokeza asubuhi na mapema ya Mei 7.2017 na kupiga kura katika duru ya pili na ya mwisho ya uchaguzi huo wa rais.
Rais huyo mteule mwenye mlengo wa msimamo wa wastani huku aliyekuwa akichuana nae kwa karibu Marine Le Pen a mbaye alikuwa mrengo wa kulia, wametokea katika vyama vikuu vya siasa vya nchi hiyo huku vyama vingine vikuu vya siasa, cha kisoshalisti, na cha Republicans cha kati-kulia, vilishindwa katika duru ya kwanza.
Katika upigaji wa kura, ulinzi mkali, uliimalishwa na umeendelea kuimalisha baada ya mashambulio ya kigaidi ya hivi karibuni nchini humo.
Tayari Rais wa Marekani Donald Trump, kupitia kurasa yake Twitter ameweza kumpongeza Macron kwa ushindi huo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top