Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Chelsea wainyuka Middlesbrough 3 nunge (Video)
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Ligi kuu ya soka ya England imeendelea tena Jumatatu hii ambapo vinara wa Ligi Chelsea waliinyuka Middlesbrough goli 3-0. The Blues  hao ...
Ligi kuu ya soka ya England imeendelea tena Jumatatu hii ambapo vinara wa Ligi Chelsea waliinyuka Middlesbrough goli 3-0.
The Blues  hao walishajitengenezea mazingira ya ushindi kwa kucheza kwa kujiamini muda wote wa mchezo.
Diego Costa aligeuka kuwa nyota wa mchezo baada ya kugongewa pasi murua na Cesc Fabregas katika dakika ya ishirini na tatu ya mchezo na kuipachikia bao la kwanza timu hiyo.
Mchezo ulinoga zaidi baada ya Marcos Alonso alipopachika bao lingine kwa kuunyakua mpira miguuni mwa kipa wa timu ya Middlesbrough, Brad Guzan dakika kumi na moja kabla ya kipyenga cha mapumziko .
Naye Cesc Fabregas iliingizia Chelesea goli la tatu na la lala salama.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top