Title: Bunge Sports Club yaishinda NMB
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5
Des:
Spika wa Bunge Job Ndugai akimkabidhi kikombe Naodha wa timu ya Bunge Sports Club ambaye ni Mbunge wa Mbiga, Sixtus Mapunda baada ya timu...
Timu ya Bunge Sports Club inayojumuisha timu ya mpira wa
miguu, mpira wa pete na kikapu imeibuka washindi na kunyakua vikombe
vitatu katika bonanza lililozikutanisha timu ya Bunge na timu ya benki
za NMB.
Timu ya kwanza ya Bunge kushinda kikombe ilikuwa timu ya mpira wa
pete ambayo iliifunga timu ya pete ya NMB magoli 19 kwa 2, ikifuatiwa na
timu ya mpira wa kikapu kwa wanaume ambayo iliwafunga wapinzani wao
timu ya mpira wa kikapu ya NMB kwa jumla ya vikapu 37 kwa 28.
Kikombe cha tatu kwa timu ya Bunge kilipatikana kwa timu ya mpira wa
miguu ambayo iliwafunga NMB goli 2-0 na hivyo kuendeleza rekodi ya
kutopoteza mchezo wowote ambao timu hizo zimekutana.
Timu ya Bunge Sports Club na NMB Sports Club zimekuwa zikikutana
zikicheza michezo mbalimbali zikiwa na lengo la kuboresha uhusiano baina
ya Bunge na NMB ambapo kwa mwaka huu bonanza hilo limefanyika katika
uwanja wa Jamhuri uliopo makao makuu ya nchi, Dodoma.
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Post a Comment