Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Weusi wana Utengano, Ubinafsi na Wivu – Lord Eyes
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa muziki wa hip hop ambaye aliyekua katika Kundi la Weusi, Lord Eyes, amefunguka mengi kuhusu kundi hilo baada ya kuonekana kufanya...
Msanii wa muziki wa hip hop ambaye aliyekua katika Kundi la Weusi, Lord Eyes, amefunguka mengi kuhusu kundi hilo baada ya kuonekana kufanya kazi peke yake.

Kundi hilo ambalo lilikuwa likiundwa na wasanii 5, Joh Makini, Nikki wa Pili, G Nako, Bonta pamoja na Lord Eyes, limebaki na wasanii watatu tu ambao ni Joh Makini, Nikki wa Pili na G Nako pekee.
Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM wiki hii, Lord Eyes amesikika akidai kundi hilo limejaa utengano, ubinafsi na wivu.
“Hatujawahi kuwa kwenye crews,” alisema Lord “Tuliungana kutanua wigo lakini siyo kwa mkataba wala kwanini. Weusi ni kampuni watu wanasema kila siku, ni kundi na ni kampuni ndio maana kumekuwa na utengano, ubinafsi na wivu,”
Pia rapa huyo alisema kila msanii wa kundi hilo anamiliki hisa ya asilimia 20 ya kampuni hiyo.
“Kuna maceo watano ndani ya Weusi na kila mtu alikuwa ana share yake, yanii asilimia 20/20 kila mtu. Hii asilimia 20 kila mtu ameifanyia kazi kwa sababu wigo ambao tulitaka kutanua ni kwamba twende mbele zaidi, tuwe na nguvu, umoja ni nguvu, lakini haikuwa hivyo, imekuwa kama Weusi ya River Camp,” alisema Lord.
Lord Eyez pia aliachia wimbo wake mpya ‘Hela Yangu’, aliyoifanya chini ya msaada wa Barakah The Prince.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top