Yapata miaka zaidi ya 7, tangu klabu hiyo kushiriki michezo yoyote katika Makao makuu ya nchi, na hatimae wakazi wa Jiji hilo watawashuhudia wachezaji wa klabu hiyo mubashara, huku wakijitupa uwanjani kuvaana na klabu ya Soka ya Polisi.
Yanga wameshatua katika mkoa huo jioni ya jana, na kufanikiwa kufanya mazoezi mepesi mepesi katika kujiweka sawa kuwavaa Maafande. Katika mechi hiyo, kutakuwa na michezo mingine pia, yakiwemo timu ya Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania wakicheza dhidi ya Baraza la wawakilishi visiwani Zanzibar, na kwa upande wa Mchezo wa Mpira wa Pete timu ya Bunge wanawake watavaana na Baraza la wawakilishi kutoka Zanzibar.
Hizi ni sherehe za 53 za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo historia yake iliundwa mnamo tarehe 26 Aprili, 1964 kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja).
Ifikapo 26 Aprili, kila mwaka, Tanzania imekuwa ikiadhimisha sherehe za Muungano kwa shughuli za kitaifa.
Post a Comment