Kikosi hicho kinachoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza nyuma ya klabu ya Chelsea inaahidi kulinda wachezaji wake wasije wakachukuliwa na klabu nyingine zilizoanza kunyemelea katika kikosi hiko.
Pochettino amesema kua ana mahusiano mazuri na mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy ambae amemuhakikishia klabu hiyo haitauza wachezaji wake na kamwe haina haja na fedha, na kuongeza, wachezaji wao watasalia ndani ya klabu amesema.
Beki wa kikosi hiko, Kyle Walker na Danny Rose pamoja na viungo wa kati Christian Eriksen na Dele Alli ni miongoni mwa wachezaji wanaosemekana kukikacha kikosi hiko cha White Hart Lane, suala ambalo liawaumiza vichwa uongozi wa klabu hiyo.
Meneja huyo amesema kua ,wanadhani kuwa wanafanya mambo mazuri na ndio sababu klabu nyingi zenye uwezo zinawatolea macho wachezaji wao wenye vipaji vikubwa
Post a Comment